Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18,
2017 akizungumza Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu
katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu
katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakimsikiliza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18,
2017 wakati wa kikao cha kuimarisha utendaji
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda wakati wa kikao cha Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu
katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Leo Mei 18,
2017.
Baadhi ya Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu
katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakifuatilia kikao cha kazi kilichoongozwa na Rc Makonda
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18,
2017 akizungumza Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu
katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia
katika utendaji wao.
1.Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi
Kushughulikia migogoro ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi wasipeleke
malalamiko yao ngazi za juu.
2.Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na
Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja Na zoezi
hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017. Mwanzoni mwa mwezi wa Saba
kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi
kwenye mtandao Jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa
wananchi.
3.Wakuu wa Idara katika Sekta ya Ardhi Na Ujenzi
kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara kwenye vyombo vya
habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana mahusiano Na
waandishi mbalimbali katika vyombo vyombo vya habari.
4.Wakuu wa
Idara ya Ardhi Na Ujenzi kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi
yaliyotolewa Hati, Na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo
ya wazi kama wapo.
5.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kusimamia
haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama kama vile Shule, Hospitali,
Na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba Na kutoa Mikakati
wa Upimaji.
6.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha
ufanisi Na bidii ya utendaji inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha
wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa vyema Madiwani
watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya Ardhi.
7.Kushughulikia changamoto za kisera unaofanya utaratibu wa Upimaji Na utoaji wa Hati kuchelewa kukamilka.
8.Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa Na utendaji imara unaoshabihiana Na Jambo la kisera.
9.Kila Mtumishi kufanya Kazi yake kwa Uaminifu kwani dhamani aliyopewa
ni kubwa Na anapaswa kuitendea Haki. Watumishi wote kusimamia Na
kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho
kimeingia mkataba Na wananchi katika kipindi cha miaka mitano.
10.Kila Mkuu wa Idara kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya
Mwaka 2015-2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake
sambamba Na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma Na kuielewa vyema
ilani hiyo.
11.Kufatilia Na kufahamu upandaji wa madaraja Na
stahiki zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja Na
kwenda likizo.
12.Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo Na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika.
13. Kuwa Na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi.
14.Kujitokeza ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi
waliojihusisha Na utoaji wa Hati za Ardhi kinyume Na sheria. Na endapo
wasipojitokeza Na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.
15.Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze kuelewa. Sambamba Na
kutoogopa maadhimio kama wanatenda Kazi kwa mujibu wa Sheria pasipo
kupendelea.
16.Wakuu wa Idara kila mwisho wa wiki kutoa taarifa kwa Wakurugenzi inayoonyesha idadi ya Migogoro Na jinsi ilivyotatuliwa.
17.Katika kupunguza changamoto ya kuwafikia wananchi kwa Wakati RC
Makonda Amesema atatoa Pikipiki 5 Katika Sekta ya Ardhi kwa kila
Manispaa.






0 Comments