Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akitembelea shamba la mfano la zao la biashara la korosho lililopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,amemaliza ziara
yake ya kutembelea wilaya sita kimkoa,ambapo amehimiza mambo makuu manne
ikiwemo ulinzi na usalama,uwekezaji,kilimo cha matunda na korosho.
Aidha amekemea migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa
ikigharimu maisha ya watu na wengine kujeruhiwa pasipo sababu za msingi.
Akimaliza ziara yake wilayani Kibaha,mhandisi Ndikilo,alieleza
mkoa wa Pwani una viwanda vitatu vikubwa vya kusindika matunda kwa sasa ambavyo
endapo wakulima watavitumia watanufaika kwa kiasi kikubwa.
Alisema,kiwanda cha Bakhresa ambacho kipo Mwandege -Mkuranga
kimeshaanza kazi na kile cha Elven Agri co.ltd kilichopo kata ya Mapinga
-Bagamoyo huku cha Sayona
kinachojengwa kata ya Mboga kikiwa kwenye hatua za mwisho za ujenzi.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kiwanda cha kusindika matunda cha
Bakhresa kina uwezo wa kusindika tani 350 za matunda kwa siku na uwekezaji wake
umegharimu sh.bil.261.
Mhandisi Ndikilo alisema uwekezaji wa viwanda hivyo ni mkubwa na
utawatengenezea kipato na soko wakulima wa matunda .
“Niwasihi wakulima wa mkoa wa Pwani na mikoa mingine kulima kwa
bidii maembe,nyanya,mananasi,mapeasi ,pilipili “
“Sio tu mlime kwa kilimo chetu tulichokizoea ,hapana kwasasa inabidi
twende na mabadiliko ya teknolojia ya kisasa kwa kutumia mbegu,pembejeo bora na
mpalilie na kutumia madawa ili kupata matunda yatakayouzika”alifafan ua.
Hata hivyo mhandisi Ndikilo aliwaomba wawekezaji wa ndani na nje
ya nchi kukimbilia kuwekeza mkoani Pwani kwani unaelekea kuwa ukanda wa
viwanda na uwekezaji.
Alisema kwasasa viwanda vilivyopo ni 200 ambavyo vipo
vikubwa,vidogo na vya kati na mabavyo vimeanza kazi,vinavyoendelea na mchakato
na vingine hatua za mwisho za ujenzi .
Akizungumzia masuala ya ulinzi na usalama ,aliwataka wananchi kila
mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake na kuacha kuamini wageni wanaoingia katika maeneo
yao.
“Ukiona kuna mtu yupo kijijini ama kwenye mtaa wako humjui na
unamtilia shaka basi toeni taarifa kwenye vyombo vya dola ili viweze
kumfuatilia”
Hakusita kukemea migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa
ikigharimu maisha ya watu kwa kujeruhiwa ma kupoteza maisha.
Kwa mujibu wa mhandisi Ndikilo,migogoro hiyo haina tija miongoni
mwao na kusisitiza umoja,upendo na amani katika pande hizo mbili .
Alisema wamejipanga kuongea na mhimili husika ili kuuomba kumaliza
migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kutoa hukumu badala ya kupiga faini.
Mhandisi Ndikilo alisema wafugaji wakitozwa faini wamekuwa na
kiburi na dharau kutokana na kuwa na uwezo wa kulipa hivyo kuanzia sasa wapigwe
kifungo ili kukomesha jeuri yao.
Katika hatua nyingine amewataka wazazi na walezi kusomesha watoto
wao wa kike na wakiume pasipo kuwabagua kwani elimu ni ufunguo wa maendeleo ya
maisha yao ya baadae.
Nae katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji mkoani
Pwani,Shangwe Twamala alisema ziara hiyo ililenga kutembelea maeneo yenye
uzalishaji wa mazao ya kilimo cha biashara kama kwenye maghala ya korosho na
viwanda vya matunda.
Pia kutembelea mashamba ya wakulima wa mihogo na kuhimiza kilimo
kinachostahimili ukame ikiwa ni pamoja na mhogo,mtama,mikunde na viazi vitamu.
Twamala alisema wananchi wanapaswa kujiwekea utaratibu wa kucheza
na misimu ya mvua kwa kulima mazao yanayotakiwa ili kukabiliana na uhaba wa
njaa.
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Ndikilo
alitembelea maeneo ya Mji wa Rufiji,Mkuranga,Kibiti,Bagamoy o,Chalinze,Kisarawe
na Kibaha.

0 Comments