Mjumbe wa Kamati ya usajili ya Singida United Fc, Festo Sanga akimkabidhi Nhiv Simbarashe jezi namba 11 ya Singida United
Mjumbe wa Kamati ya usajili ya Singida United Fc, Festo Sanga akimsainisha Mzimbabwe huyo Nhiv Simbarashe.
Ni kama ndoto, lakini ni kweli moja ya
timu zilizopanda daraja mwaka huu (SINGIDA UNITED FC) imekuja kivingine
takribani miongo kadhaa tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mbali ya maandalizi ya uwanja, basi na usajili wa kocha tishio nchini
Mholanzi Hans Vn de Pluijm.
Jana majira ya mchana,Singida United Fc
wameinasa saini ya mshambuliaji mzoefu aliyeitoa TP MAZEMBE kwa goli
pekee mwezi uliopita kwenye michuano ya Club Bingwa Barani Africa si
mwingine ni Mzimbabwe, Nhiv Simbarashe.
Mshambuliaji huyu wa timu ya Taifa ya
Zimbabwe kwa nyakati tofauti na aliyezichezea super sport na Mamelodi
Sundowns zote za Africa Kusini kwa mafanikio makubwa na baadae kutua
Caps United ya Zimbabwe ambayo hadi sasa ndio anamaliza mkataba wake na
kuamua kutimukia Singida United kwa kandarasi ya miaka miwili.
Simbarashe anakuwa mchezaji wa tano wa
kimataifa kusajili na Singida United tayari kwa msimu wa VPL
2017/2018.Waliokwisha sajiliwa awali ni wazimbabwe Twafaza
Kutinyu,Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Mganda Shafik Batambuze.
Usajili huu unaonesha wazi Singida
United hawajaja Ligi Kuu kushiriki bali kutafuta Ubingwa na baadae
kwenda kwenye Ligi ya mabingwa barani Africa. Ni hatua nzuri kwa soka la
nchi yetu kuona timu ndogo zinafanya mambo makubwa ambayo
hayakutarajiwa na wengi,tunawatakia kila raheli Singida United Fc katika
maandalizi yao (pre season) yanayoanza pale mwanza tar.12/06/2017.


0 Comments