Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio zao katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay
Washiriki wakivishwa medali baada ya kumaliza kukimbia katika mashindano hayo
Elizabeth wa NMB Bank akivishwa medali baada ya kumaliza mbio hizo.
ni mbio kwa kwenda mbele
Mshiriki akiangalia muda alioutumia kukimbia. Kushoto ni Mwanariadha nguli wa zamani Juma Ikangaa
Juma Ikangaa akiwavisha medali washiriki wa mbio hizo
Mtoto akiwa miongoni mwa wakimbiaji
Wakimalizia kukimbia
Wakiendelea na mazoezi baada ya mashindano
Timu ya NMB Bank iliyoshiriki katika mashindano hayo
Wakifurahia kumaliza mbio
Juma Ikangaa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mbio za wanawake umbali wa Km 10, Mary Naari
Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 10 wanaume, Sylvester Simon akikabidhiwa zawadi na Juma Ikangaa
Dorothy Kipeja wa Dar Running Club waandaji wa mashindano hayo, akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Km 21
Mshindi wa kwanza wa mbio za umbali wa Km 21, Augustine Sule
akipongezwa na Juma Ikangaa alipokabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa
Michezo, Yusufu Singo (wa pili kulia)
Mshindi wa kwanza kwa upande wa walemavu Shukuru Khalfan
(katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Michezo, Yusufu Singo pamoja na
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza, Nalaka.
Nahodha wa timu ya riadha ya Radio EFM, Maulidi Kitenge
akiwapongeza waandaji wa mashindano hayo baada ya timu hiyo kushiriki
ipasavyo.
Mtoto aliyeshiriki na kumaliza vizuri mbio hizo, akizawadiwa soda
Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusufu Singo (kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya mbio ya Km 21 ya Dasani
Marathon 2017 baada ya kuwakabidhi zawadi zao eneo la Bwalo la Maofisa
wa Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo. Mshindi wa kwanza, Augustine Sule
(aliyesimama juu), Mshindi wa pili Stephano Huche (wa pili kushoto) na
mshindi wa tatu Said Makula. Kushoto ni Nalaka Hettierachchi Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza iliyodhamini mashindano hayo
kupitia kinywaji cha maji ya Dasani.
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa
na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amefurahishwa na mashindano ya mbio
ya Dasani Marathon 2017 yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa kupitia
kwenye hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Michezo wa
wizara hiyo, Yusufu Singo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa
mashindano hayo yenye umbali wa Km 10 na 21.
Pia aliipongeza Klabu ya Dar
Running Club kwa maandalizi mazuri yaliyofanikisha mashindano hayo
yanayodhaminiwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza kupitia maji ya Dasani.
Kampuni hiyo imeingia mkataba wa kuyadhamini mashindano hayo kwa miaka
mitano.
“Nawapongeza nyote kwa kuchukua
jukumu kubwa la kufanikisha maandalizi ya mbio hizi ambayo siyo tu ni
nzito bali muhimu katika mchakato mzima wa kujenga utamaduni wa kuzijali
afya zetu na ustawi wa familia zetu, uelewano uliothabiti katika
kutekeleza majukumu yetu ya kifamilia na kitaifa”. Alisema Mwakyembe.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa
Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza, Nalaka Hettierachchi alisema
wanataka mashindano hayo yawe makubwa ambapo hivi sasa wana mipango ya
kuyapeleka pia katika mikoa mingine nchini.
Mashindano hayo yaliyoshirikisha
zaidi ya watu 1000 kutoka maeneo mbalimbali nchini, yalianzia na kuishia
Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay na kupita barabara mbalimbali za
Jiji la Dar es Salaam ikiwemo ya Ali Hassan Mwinyi.
Aliyeibuka kidedea katika mbio za
wanaume za umbali wa Km 21 ni Augustine Sule, wa pili akiwa Stephano
Huche na Said Makula aliyeshika nafasi ya tatu.
Kwa upande wa Wanawake aliyeibuka
mshindi ni Jacquline Sakilu, wa pili akiwa Noela Remmy na nafasi ya
tatu ilikwenda kwa Antery John.
Kwa mbio za umbali wa Km 10,
mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa Sylvester Seleman, wa pili akiwa
Daniel Sinda na Paul Pascal alishika nafasi ya tatu.Mshindi wa kwanza
kwa wanawake alikuwa May Naari, wa pili akiwa Sara Hitis na Asia Seleman
aliyetwaa nafasi ya tatu.
Kwa upande wa walemavu aliyeshinda ni Shukuru Khalfan, wa pili alikuwa Mathias John na Jonis Stephano alishika nafasi ya tatu.
Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 21
kwa upande wa wanaume na wanawake kila mmoja alikabidhiwa sh. mil 1, wa
pili sh. 750,000 na wa tatu sh. 600,000.

0 Comments