Simba imeingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambao una thamani ya Sh bilioni 4.9.
Mkataba huo, utaifanya Simba ipokee kitita cha Sh milioni 888 katika mwaka wa kwanza.
Mmoja wa Wakurugenzi
wa SportPesa, Abbas Tarimba amesema Simba itapewa Sh bilioni 1 na
milioni 80 katika mwaka wa mwisho wa mkataba kwa kuwa kila mwaka, fedha
5% zitakuwa zinaongezeka katika mkataba.
Kama hivyo haitoshi,
Simba imepewa motisha, kuwa kama itachukua ubingwa basi ina nafasi ya
kuchukua Sh milioni 100 kama zawadi au pongezi kutoka SportPesa.
Pia SportPesa
wameonyesha wanachotaka ni kuona Simba inafanikiwa kweli, wametenga Sh
milioni 250 wakibeba Kombe la Kagame au michuano iliyo chini ya Caf.
Udhamini huo unakuwa ndiyo mkubwa zaidi kuliko mingine yoyote ambayo Simba imewahi kuingia ikidhaminiwa.
Mkataba huo unaifanya
Simba kuwa timu isiyo na hasara kama ilivyo kwa msimu huu ambao
imemaliza ikicheza bila ya kuwa na mdhamini mkuu.

0 Comments