Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bibi. Leah Kihimbi akimkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa
mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula
(kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera hiyo iliyofanyika katika
Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo
anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Macau nchini China ambapo
atashiriki mashindano hayo. Katikati ni Afisa Utumishi wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA).
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
Miss Super Model 2017 Asha Ally Mabula akizungumza wakati wa
tukio la kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi
katika mashindano ya Miss Word Super Model 2017 leo Jijini Dar es
Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China
ambapo atashiriki mashindano hayo. Kutoka kulia ni Afisa Utumishi wa
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi na Meneja Mkuu wa
Tanzania Miss Super Model Ibrahim Thabit.
Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bibi. Leah Kihimbi akizungumza wakati wa tukio la kumkabidhi
bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017,
Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo
anatarjia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki
mashindano hayo.
Baahi ya waandishi wa habari
wakishuhudia tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa Miss Word
Super Model, Asha Ally Mabula anayetarajia kushiriki mashindano hayo
Macau nchini China.
Na Nuru Juma & Husna Saidi- MAELEZO.
Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah kihimbi amemkabithi bendera ya Taifa Tanzania
Miss Super Model 2017 Asha Ally Mabula kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika
mashindano ya Dunia ya Miss Super Model
yanayotarajia kufanyika 21hadi 28 mei katika mji wa Macau nchini China.
Akimkabidhi bendera hiyo, Bi Leah alisema kuwa ana
amini Miss huyo ataenda kuliwakilisha vyema Taifa la Tanzania katika mashindano
hayo ya Dunia ambapo alimuhakikishia kuwa
Wizara pamoja na Watanzania wapo
pamoja nae kwa kipindi chote ambacho atakuwa huko.
“Mrembo wetu anatakiwa kukumbuka kuwa katika
mashindano hayo anaenda kuliwakilisha Taifa hivyo Watanzania tunamsihi asiende
kufanya vitu vitakavyoiharibu sifa ya nchi yetu
na badala yake aende kuishi kwa mila na desturi zetu za kitanzania ,”
alisema Leah.
Aidha alimsisitiza kufanya vizuri katika kuwania
taji hilo lakini pia kulitangaza Taifa
na kuweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kutangaza utalii na utamaduni wa nchi hasa
katika matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.
Naye Tanzania Miss Super Model Asha Mabula
ameishukuru Serikali kwa kuweza kumkabidhi bendera hiyo ya Taifa na ameahidi kwenda kuitangaza Tanzania katika
masuala ya utalii, kulinda heshima yake na Taifa kwa ujumla na kushiriki vyema ili kuhakikisha anarudi na
Taji la Miss World Super Model.
Hata hivyo Asha aliwaomba Watanzania kushirikiana
nae katika maombi na kuwa nae bega kwa bega kwa kila hatua atakayoifanya ili
kumpa moyo kwani anaenda kule
kuiwakilisha Tanzania na si yeye kama Asha.
Mshindi
huyo wa Tanzania Miss Super Model anatarajiwa kuondoka nchini leo kwenda Macau China kwa ajili ya kushiriki
mashindano ya Miss World Super Modal
yanayotarajia kufanyika kuanza Mei 21 hadi 28 mwaka huu.
0 Comments