Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid
Mohamed (aliyesimama katikati) akifafanua kuhusu
sursa za za uwekezaji zilizopo Zanzibar wakati wa mkutano wake na ugeni
kutoka TADB. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
hiyo, Bw. Francis Assenga (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam
Juma Abdullah (kulia).
...............
Na Mwandishi wetu,
Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid
Mohamed amesema sasa ni wakati muafaka kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
ya Tanzania (TADB) kuwekeza Visiwani Zanzibar
ili kuchagiza juhudi za Serikali za kuwawezesha kiuchumi wakazi wa
visiwa hivyo wanaojishughulisha na sekta za kilimo, uvuvi na uchakataji
mazao.
Mhe.
Hamad amesema Visiwa vya Zanzibar vina maeneo mengi ya uwekezaji yenye
kuweza kuongeza tija na ongezeko la uchumi visiwani humo ikiwa kutakuwa
na uwekezaji mkubwa katika maeneo hayo.
“Nawahakikishia,
mkianza kuwekeza katika miradi kama ya mwani, uvuvi na karafuu Bebki
itapata matokeo makubwa sana na mnaweza kuitumia Zanzibar kama mfano
rejea katika utoaji wa mikopo yenye
tija nchini,” alisihi.
Kwa
mujibu wa Mhe. Waziri, Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vyenye utajiri
mkubwa ambavyo kukiwa na uwekezaji wa kimkakati vinaweza kutokea matokeo
makubwa na yenye kuwanufaisha wananchi
wengi.
Akizungumza
na Mhe. Waziri, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga
amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB)
ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili
kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza
mapinduzi katika
kilimo nchini.
Bw.
Assenga ameongeza kuwa Benki inatambua fursa za uwekezaji Visiwani
Zanzibar na amemuahidi kuwa wamejipanga kuanza uwekezaji mkubwa wa wadau
wa sekta za kilimo
na uvuvi ambazo ni sekta za kipaumbele zinazopatiwa mikopo na TADB.
Ameongeza
kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta
hizo ili kuongeza tija sekta hizo ili kupambana na umaskini nchini.
TADB
ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu
mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo
kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa
kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi
kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo;
mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa
bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo
na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

0 Comments