Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akigawa Modem
kwa wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya
uzinduzi wa vifurushi
vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana
jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana, ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri.
Meneja
wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri (kulia) na Meneja wa
Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus wakimuonyesha
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin (wa
pili kulia) Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata
bure baada ya kujiunga na huduma mpya ya vifurushi
vya bure kwenye mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na Kampuni ya
Zantel jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Chapa
na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akisalimiana na
Meneja wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus mara baada
ya uzinduzi rasmi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam, ambapo wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki bure kupitia application ya Mdundo.com
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na
wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya
uzinduzi wa vifurushi
vya bure kwa mitandao yote ya kijamii yenye lengo la kuwanufaisha hasa
vijana. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika jana jijini Dar es salaam.
Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia
Mtingwa.
Mtaalamu
wa masuala ya Biashara Zantel, Rehene Cathbert Tarimu (kulia)
akionyesha Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata
bure mara baada ya kujiunga na huduma mpya ya vifurushi
vya bure kwa mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na Kampuni hiyo
jana jijini Dar es salaam. Katikati ni Mtaalamu wa huduma za simu
Emmilina Albert Vokolawene pamoja na Mtaalamu wa masuala ya Teknolojia
Zantel Salim Awadh.
Kampuni ya simu
inayoongoza kwa huduma za vifurushi vya intaneti, Zantel imeanzisha huduma mpya
ya vifurushi vya bure kwa wateja wake ikiwalenga zaidi vijana, ambapo tafiti
zinaonyesha ndio watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii.
Akizindua rasmi huduma hiyo jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Bw. Benoit Janin amesema wateja wa Zantel
wanaojiunga na vifurushi vyetu vya kila siku, wiki na mwezi watapata nafasi ya
kutumia mitandao ya Facebook, Twitter pamoja na huduma ya kusikiliza muziki
bure kwenye application ya ‘Mdundo.com’.
Aliongeza kwa kusema “Tunajisikia fahari kubwa
sana kuweza kuzindua huduma hii mpya ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zetu za
kupanua na kutoa huduma za kibunifu na kuhakikisha wateja wetu wanaendelea
kufurahia mtandao wetu wa Zantel wenye huduma ya intaneti ya kasi zaidi ya 4G
Tanzania nzima.
Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo, Mkuu wa
kitengo cha huduma ya Vifaa na intaneti Zantel, Hamza Zuberi alisema, “Kwa
wateja wa Zantel watakaonunua vifurushi vya siku, wiki na mwezi ambavyo ni
;-Sh.500/= kwa 500MB, Sh.1000/= kwa 1.2GB, na Tsh.1500/= kwa 2.5G watapata
nafasi ya kufurahia huduma hizo za bure. Huduma hizi ni kwa wateja wenye simu
au vifaa vyenye uwezo wa kupokea huduma ya intaneti. Kwa wateja wetu wanaotumia
simu au vifaa visivyo na uwezo huo wanaweza kujipatia simu au vifaa hivyo kwa
gharama nafuu kabisa katika maduka ya Zantel jijini Dar es Salaam na visiwani
Zanzibar ili na wao waweze kufurahia ofa hii”.
Aliongeza kuwa baada ya kufanya utafiti wa
kina kwenye soko la mitandao ya simu waligundua kuwa vijana wengi wanapenda
muziki ambapo mpaka sasa hakuna kampuni yoyote ya simu inayotoa huduma hiyo bure,
na hivyo kuwafanya Zantel kuileta huduma hiyo sokoni kwa kupitia ‘Mdundo Music
Application.’
‘Mdundo Music Application’ ni moja ya programu
kubwa kabisa za muziki barani Afrika inayowawezesha watu kuweza kusikiliza aina
zote za muziki kwa kutumia intaneti. Programu hiyo ina zaidi ya nyimbo 200,000
kutoka kwa wanamuziki zaidi ya 40,000. Zantel inaamini ofa hii itawafaa zaidi
vijana kwakuwa wengi wao wamekuwa kwenye utamaduni wa kisasa unaopenda ziaidi
muziki na hivyo huduma hii ya bure itawavutia zaidi.
Aliongeza kuwa huduma hiyo mpya inapatikana
karibu kwenye mifumo yote ya simu za mkononi kama vile Android, iOS kwa ajili
ya iPhone, Blackberry na Nokia Symbian.
Martin Nielsen, Afisa Mtendaji Mkuu wa
Mdundo.com alisema, "Wateja wa Zantel wanaweza kupata orodha yote ya
nyimbo kupitia Mdundo ikiwa ni pamoja na nyimbo mchanganyiko zilizoandaliwa na Ma
DJ maarufu, muziki wa Afrika Magharibi na pia Mashariki. Tanzania ni soko letu
ambalo linakuwa kwa kasi sana na tunatarajia kuwa
mpango huu utasaidia kupunguza kiwango kikubwa cha uharamia kwenye soko la
muziki nchini na kuwapa wateja sababu ya kufurahia muziki zaidi ya hapo awali”.
Huduma hii mpya kutoka Zantel imekuwa
miongoni mwa huduma nyingine za kibunifu na kidijitali ambazo zimeanzishwa na
Kampuni hiyo hivi karibuni. Huduma hizo ni pamoja na uzinduzi wa mtandao wenye
kasi wa 4G LTE upande wa Bara na Visiwani, 'Zantel Madrasa' huduma
inayowawezsha waumini wa dini ya Kiislamu kupata mafundisho, Quran, Habari za
BAKWATA na mawaidha mbalimbali ya kiislamu kwa njia ya simu, ikiwemo pia kwa
njia ya SMS na ‘ Zantel Madrasa App’.
Akizungumzia uwekezaji wa Zantel, Janin alisema wamewekeza zaidi
ya dola za kimarekani milioni 10 katika uboreshaji wa mtandao ambapo mpaka sasa
zoezi la maboresho hayo katia maeneo ya Stone Town Zanzibar na Mkoa wa Mjini
Magharibi yameshakamilika. Zoezi hilo linaloendelea hivi sasa katika
visiwa vya Unguja na Pemba linaarajiwa kufikia
kikomo mwisho wa mwezi huu.






0 Comments