Washindi wa makapu katika picha ya pamoja wakisubiria kukabidhiwa makapu yao
Makapu ya Eid el-Fitri yakiwa yamesheheni vyakula mbalimbali
Washindi wa makapu katika picha ya pamoja wakisubiria kukabidhiwa makapu yao
Mwigizaji mashuhuri Riyama Ally ambaye ni balozi wa Dstv akimkabidhi mshindi Benjamin n osha kapu lake la Eid el-Fitri’
Meneja wa vipindi wa Efm radio Dickson Mponela akimkabidhi moja ya washindi Rebeca Lukule kapu lake la Eid Al Fitri
Katika kuelekea sikukuu ya Eid el-Fitri, E-FM Radio imetoa zawadi
kwa wasikillizaji wake kama ilivyo tamaduni yake ya kutoa kwa jamii,
ambapo wasikilizaji 10 kutoka jijini Dare s salaam waliofanikiwa
kusikiliza redio na kujibu maswali kuhusu kampeni ya Kapu la sikukuu
wameondoka na makapu yalioyo sheheni vitu mbalimbali ikiwemo vyakula
muhimu kwa ajili ya sikukuu hiyo.
Tukio hilo
limefanyika leo siku ya Jumamosi ya tarehe 24/06/2017 katika ofisi zao
zilizopo Kawe – beach.DSTV nao waliongezea nakshi kwenye kapu kwa
kuwazawadia washindi wa makapu ya sikukuu ving`amuzi vyao na kuwapa
kifurush cha mwenzi moja bure. Zoezi hili litaendeshwa pia
kwa washindi kutoka jijini Mwanza ambako EFM Radio inasikika kupitia
masafa ya 91.3. washindi hao watajipatia zawadi zao za Kapu la sikukuu
siku ya Jumapili tarehe 25/06/217 kwenye ofisi za DSTV Kenyata road
Mwanza.




0 Comments