SERIKALI imeelezwa kuwa kwakiwango kikubwa mazingira ya kujifunza na kufundishia bado si rafiki kwa moto wa kike , kwa mujibu wa takwimu za BEST(BasicUducatin Statics) za mwaka 2016, zimetaja kuwa kunaupungufu wa mkubwa sana wa matundu ya vyoo ambapo wasichana 52 wanalazimika kutumia tundu moja la choo badala ya wasichana 20 kutumia tundu moja la choo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Elimu Nchini , John Kalaghe (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuondoa Vikwazo kwa Mtoto wa Kike katika hafla iliyofanyika katika ofsi za Tasisi hiyo Upanga jijini Dar es Salaam Juni 20, 2017.Kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa kwa jamii kumpa fursa msichana hili aweze kupata mafanikio na kufikia maelengo yake (katikati), Msemaji kutoka TGNP, Grace Kisetu .
Ukosefu wa maji pia ni tatizo kwani
asilimia 43.6 ya shule za msingi
na asilimia 54.4 ya shule za sekondari tu ndiyo zina huduma ya maji,
hali ya ukosefu wa vyoo
na maji katika shule
,inahatarisha afya zao na kuwaweka katika
hatari ya kupata magonjwa yohusiana na uchafu.
Akizunguza Dar es Salaam jana kwenye uzinduzi wa
kampeni maalumu ya kuhamasisha ufanikishaji wa elimu ya moto wa kike Mkurugenzi
Mtendaji wa Hakielimu John Kalage alisema kuwa kampeni hiyo inatokana na
ongezeko kubwa la changamoto za
kimazingira,kiutamaduni,kiuchumi na
kimazoea ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma
sana haki za ya upatikanaji wa elimu bora kwa motto wa kike nchini.
Alisema kuwa kumekuwepo
na taarifa nyingi za unyanywasaji ambazo kwa kiwango kikubwa mwasilika
amekuwa ni motto wa kike, athari za unyanyasaji
huo ni mkubwa na zinahitaji juhudi za pamoja ili kuweza kumkwamua motto
wa kikike katika hatari ya kukosa
haki yake kupata elimu bora na kufikia
ndoto zake kama mwanadamu na kama raia yeyote mwingine wa Tanzania.
“Kwa kutambua hilo ,suala la ulinzi wa motto husuani motto wa kike na wale wenye
mahitajia maalum ni suala ambalo
hakielimu imelipa kipau mbele katika
mpango mkakati wake mpya wa mwaka
2017 hadi mwaka 2021 ambapo kampeni hiyo inachagizwa na ukweli kuwa elimu ya motto wa kike
inachangamoto mali mbali ambazo hazina budi kutatuliwa ili kuwezesha watoto wa
kike kuwa shuleni na kupata elimu
bora,”alisema Kalage.
Kalage alisema niwazi
kuwa kwa sababu ya maumbile ya kibaiolojia motto wa
kike ana mahitaji zaidi ya motto wa kiume hata hivyo kutokana na sababu za kukosa vifaa kama taulo
za kike kwa ajili ya kuwasaidia katika
siku zao,watoto wengi
wa kike hushindwa kuhudhulia shule
na kuamua kukaa nyumbani
hadi siku zinapoisha.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa utafiti wa SNV wa mwaka 2015 umeonesha kuwa asilimia 25
tu wa wasichana waliohusika katika
utafiti ndio hupata vifaa na kuwa
umebainisha kuwa njia madala kwa wasichana
wasiopata vifaa ni kuamua kukaa
nyumbani kati ya siku 4-5 ili kujisitiri
na kuwepo aibu.
Alisema uchunguzi wa
HakiElimu kwa kutumia takwimu
za BEST takribani wasichana
700,000 hadi 750,000 wa darasa la sita na saba
hupoteza siku 40 hadi 50 kati ya
siku 290 za mwaka wa masomo ambapo hali
hiyo ufanya watoto wake kukosa vipindi
vya kujifunza mada mambali mbali.
“Ripoti ya Human Rights
Watch ya mwaka 2017 yenye kichwa cha habari(I had aDream to Finish
School) imebainisha changamoto lukuki za unyanyasaji wa kijinsia kwa
watoto wa kike kama vile walimu
kuwataka wanafunzi wa kike
kimapenzi na kuwavisha kuwaadhibu
wanapokataa kufanya mapenzi na walimu,”alisema .
Aidha alisema kuwa unyanyasaji wa wanafunzi wa kike
imebainishwa kuwa madhara wanayoyapata watoto wa kike kwa kufanyiwa
unyanyasaji na jinsi unavyo waathiri kisaikolojia na kufanya washindwe kuzingatia elimu yao wawapo
shuleni.
Pia uhaba wa mabweni
na changamoto za usafiri huwaadhiri
pia watoto wa kike katika elimu ya
sekondari, shule nyingi za kata ziko mbali mbali na makazi,ripoti ya
HumanRights Watch ya mwaka 2017
imebainisha kuwa changamoto za usafiri
huwafanya wasichana kulazimika kufanya mapenzi na madereva wa magari au pikipiki ili kupata urahisi wa
kufika ki;la siku shuleni na matokeo yake upata ujauzito na kufukuzwa shule.
0 Comments