Mwenyekiti
wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta (kulia) akizungumza na
vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha
miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano
ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa
kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa Julai
08. Katikati ni Meneja Msaidizi wa klabu hiyo, Elizabeth Michael na kushoto ni
Mratibu wa Masoko na Matukio Levina George.
Meneja
wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula
Gambalagi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
kuhusiana na udhamini wa mashindano yatakayosindikiza maadhimisho ya miaka 100
ya klabu ya Dar es Salaam Gymkhana tangu ilipoanzishwa mwaka 1916. Katika
kuadhimisha siku hiyo ya kihistoria, klabu imejipanga kuandaa michuano ya
michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa
kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe
Julai 08.Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ndio mdhamini Mkuu wa mashindano
hayo. Wadhamini wengine wa mashindano hayo ni pamoja na Clouds Media Group,
Qatar Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance brokers, Vodacom
na Mwananchi Communications.Kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam
Gymkhana, Walter Chipeta.
Mwenyekiti
wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta (katikati) akisikiliza
maswali toka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano
uliofanyika leo jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka
100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya michezo
mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na
mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08.
Kulia ni Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula
Gambalagi na Meneja Msaidizi wa klabu hiyo, Elizabeth Michael (kushoto).
Mwenyekiti
wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta akisalimiana na Meneja
wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula
Gambalagi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari jana jijini Dar es
salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake
mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu,
Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa
kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08.
.........................................................
Klabu
ya Gymkhana Dar es salaam inayojihusisha na michezo ya aina mbalimbali
imejipanga kusherehekea kutimiza miaka 100 kwa staili ya tofauti tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1916.
Katika
kuadhimisha tukio hilo la kihistoria, Klabu hiyo imeandaa idadi ya michezo
mbalimbali itakayosindikiza maadhimisho hayo ambapo michezo hiyo inatarajiwa
kuanza tarehe 03 Julai, 2017 na kuhitimishwa tarehe 08 Julai kwa mujibu wa Mwenyekiti
wa klabu hiyo, Bw. Walter Chipeta.
Miongoni
michezo iliyopangwa kufanyika katika kuadhimisha miaka 100 ya klabu hayo ni
pamoja na Gofu, Tenisi, Skwashi, Soka, Kriketi, mchezo wa kuogelea na mingine
mingi ambayo kwa ujumla itawahusisha wanachama na wasio wanachama wa klabu
hiyo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar
es salaam, Mwenyekiti wa Klabu ya Gymkhana, Walter Chipeta alisema,
“Maadhimisho ya miaka 100 ni tukio la kihistoria kwa ajili ya klabu yetu na
tumejipanga kusheherekea shughuli hii kupitia michezo mbalimbali ambayo itaanza
rasmi tarehe 03 Julai na kilele chake kuwa tarehe 8 Julai.”
Chipeta
alisema klabu hiyo inawakaribisha wanachama na wasio wanachama kutoka ndani na
nje ya Tanzania ili kushiriki kwenye maadhimisho hayo na kusisitiza kwamba
washiriki watafurahia na kuburudika.
Kwa
upande wake Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao ndio
wadhamini rasmi wa maadhimisho ya miaka 100 ya Gymkhana Ndg. Itandula Gambalagi
alisema, “Tunajisikia fahari kuhusishwa na klabu kubwa kama hii na kwenye tukio
la kihistoria kama hili la kuikumbuka klabu hii kongwe. Aliongeza kuwa tukio
hilo litatoa fursa kwa NHC kujitangaza zaidi na kukutana na wateja wake muhimu
katika mazingira tulivu ya kijamii.”
Licha
ya NHC kuwa wadhamini rasmi wa shughuli hiyo, Klabu ya Gymkhana pia ilitoa
shukrani kwa wadhamini wengine wa mashindano hayo ambao ni pamoja na Clouds
Media Group, Qatar Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance
brokers, Vodacom na Mwananchi Communications.
Klabu
ya Dar es Salaam Gymkhana ikiwa ni kituo au sehemu ya kukuza michezo, kwa miaka
mingi imekuwa ni chombo muhimu kinachowaunganisha watu kupitia michezo na
shughuli mbalimbali za kijamii.
Pia,
imekuwa ikiendesha michezo ya watoto na watu wenye ulemavu ambao pia wanapata
fursa ya kushiriki michezo kama tenisi na Skwashi.
Hii
ni klabu ambayo inapokea watu wote wanaopenda kuwa sehemu ya jumuiya ya wapenda
michezo na kuwa sehemu ya maadhimisho haya ya kihistoria ili kuendelea kukuza
michezo mbalimbali.




0 Comments