Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe, Ferdinand Wambali wa akisalimiana na baadhi ya
watumishi wa Mahakama ya
Wilaya ya Kasulu mara
baada ya kuwasili katika Mahakama hiyo hivi karibuni, wakati alipotembelea Mahakama hiyo na kufanya ukaguzi wa shughuli za utendaji kazi na miundombinu ya Mahakama.
Na Magreth
Kinabo - Mahakama ya Tanzania
Jaji Kiongozi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinad Wambali amesema kwamba mkoa wa Kigoma utapatiwa
Mahakama Kuu hivi karibuni,ikiwa ni
hatua ya kuwaondolea adha wanaoipata
wananchi ya kutafuta huduma ya mahakama
hiyo kutoka eneo moja hadi jingine
Kauli hiyoimetolewa tarehe mwishoni mwa wiki
iliyopita na Jaji Kiongozi wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Kibondo kuhusu malengo ya
ziara yake katika mkoa wa Kigoma,hivyo aliwataka baadhi
ya viongozi na wananchi kuvuta subira.
Jaji Kiongozi , pia alizungumza na baadhi ya viongozi
waandamizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, wakiwemo baadhi ya watumishi wa
Mahakama Kuu kutoka kanda hiyo
ambayo inajumuisha mikoa miwili yaani na Tabora na Kigoma.
“Tayari kiwanja kimeshapatikana na eneo la Buhigwe na tenda imeshatangazwa, hivyo mchakato wa
ujenzi utaanza hivi, karibuni,”alisema Jaji Kiongozi.
Kiwanja hicho
kina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 16,000.
Mkoa huo,
unahitaji huduma ya Mahakama Kuu kwa sababu ya kukua kwa idadi
ya watu,pia hivi sasa watu wanatoka
katika mkoa huo kwenda kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoa wa Tabora , pia kukua kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Jaji Kiongozi
aliongeza katika kanda hiyo, wilaya ambazo hazina mahakama za wilaya zitajengewa mahakama kwa
kuwa Mahakama ya Tanzania kupitia mpango
Mkakati wa Miaka Mitano(2015/16 hadi 2019/20
imejipanga kujenga mahakama kila wilaya, tarafa na kata.

0 Comments