Spika wa Bunge, Mhe. Job
Ndugai, pamoja na Mwenyekiti wa Mtandao wa Kuondoa Umasikini Ndg. Mungwe
Athuman (kulia) wakimkabidhi kitabu Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari
Manghweta Ndg. Elinetha Kimaro (kushoto) wakati wakigawa vitabu Mbali mbali kwa
Shule za Sekondari zilizopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe Job
Ndugai (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Mtandao wa Kuondoa Umasikini
Ndg. Mungwe Athumani (kulia) wakikabidhi vitabu kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya
sekondari Iduo Ndg. Cathbert Kalindo, Shule iliyopo Wilaya ni Kongwa Mkoani
Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza na Wazazi
wa Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Sekondari Laikala iliyopo Wilayani
Kongwa, Dodoma wakati wa zoezi la kugawa Vitabu shuleni hapo vilivyotolewa na Mtandao Kuondoa Umasikini, kushoto
ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai
(wa tatu kulia) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ibwaga iliyopo
Wilayani Kongwa, Dodoma baada ya kugawa vitabu shuleni hapo, vitabu hivyo
vimetolewa na Mtandao wa kuondoa Umasikini. Kulia kwa Spika ni Mweyekiti
wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athuman na
kushoto kwake ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa. Zoezi la ugwaji wa
vitabu hivyo lilianza toka wiki
iliyopita ambapo takribani shule thelathini za Sekondari zilizopo Wilaya ya
Kogwa, Dodoma zimenufaika na msaada huo.




0 Comments