Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto)
akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen
Magoiga wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani kulia ni Kamanda wa
Polisi mkoa huo, Muliro Jumanne Muliro.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack
akiangalia mashine za kukoboa na kusaga nafaka pamoja na kusindika alizeti kutoka
mjasiriamali Mzee Nassoro alipokuwa kata ya Mwamamalasa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia)
akiwa na Katibu Tawala Mkoa, Albert Msovela (katikati) pamoja na Katibu Tawala
Wilaya, Shadrack Kangese (kushoto) wakati wa ziara.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto)
akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen
Magoiga.
Mjasirimalia Mabela Msolwa kutoka wilayani Kishapu
akitoa maelezo kuhusu mradi wake wa mashine za kuchakata nafaka na ghala kuhifdhi nafaka kwa Mkuu wa mkoa (kulia) na
viongozi wengine wakati wa ziara hiyo.
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kishapu, Lucas Said
(kushoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa huduma ya maji ya Ziwa Victoria kwa
wananchi kata ya Maganzo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia)
akitoa maelekezo wakati alipotembelea ghala la nafaka la Mabela mjini Mhunze
kata ya Kishapu wakati wa ziara yake.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia)
akifafanua jambo kwa viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo kijiji cha
Kinampanda kata ya Mwamalasa.
Na Robert Hokororo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya
ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma
ya maji kutoka Ziwa Victoria uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa
zahanati kata ya Shagihilu.
Mradi mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika
alizeti na kukoboa nafaka za mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa
hivi karibuni.
Kwenye kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea
mradi mwingine wa ghala la kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za
mahindi na mpunga.
Katika ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na
Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa
akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.
Alikaribishwa na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga
Talaba, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu
wa idara katika halmashauri hiyo.








0 Comments