Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) unatambua kuwa baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya
kusambaza umeme vijijini hawajakamilisha miradi kwa mujibu wa MIKATABA waliyosaini na Wakala (REA). Aidha,
kuna baadhi ya wakandarasi wamekamilisha miradi lakini hawajakabidhi rasmi miradi
hiyo na vifaa au hawajafanya marekebisho kasoro zilizobainishwa na wasimamizi
wa miradi kutoka (TANESCO na REA).
Kwa tangazo hili, Wakala
unawataarifu wakandarasi wote ambao hawajakamilisha matakwa hayo ya kimikataba
kufanya hivyo mara moja. Wakandarasi watakaoshindwa kutimiza masharti hayo
hawataruhusiwa kushiriki katika zabuni zitakazotangazwa na Wakala (REA) baada
ya TANGAZO hili na hatua nyingine zitachukuliwa juu yao kwa mujibu wa mikataba
hiyo.
Imetolewa na:
0 Comments