Meneja wa mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga, akiongea na wanafunzi.
Afisa wa Masuala Endelevu ,Irene Mutiganzi akiongea na wanafunzi.
Afisa Mawasiliano ,Abigail Mutaboyerwa,akisisitiza jambo kwa wanafunzi.
Wanafunzi wakimsikiza kwa makini Afisa Mawasiliano kutoka TBL Group,Amanda Walter.
Wanafunzi
wa darasa la sita wa shule ya Oysterbay wakiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group,baada ya mafunzo ya kuchambua
changamoto za maisha wakati wa maadhimisho ya siku ya motto wa Afrika.
Katika maadhimisho ya Siku ya
Mtoto wa Afrika mwishoni mwa mwiki baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TBL
Group walijitoa kufundisha wanafunzi wa shule ya msingi ya Oysterbay iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Akiongelea maadhimisho
hayo,Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga,alisema kuwa siku hii ni muhimu
kwa kampuni kwa kuwa kupitia sera yake ya ‘Kujenga Dunia Maridhawa’ imelenga kuhakikisha inashiriki ipasavyo kuhakikisha inachangia
kukabiliana na changamoto za kijamii kwenye maeneo inayofanyia biashara lengo
kubwa likiwa ni kuifanya dunia iwe sehemu bora ya kuishi.
“Sera yetu ya Kujenga Dunia Maridhawa hailengi katika suala
la mazigira na maji pekee bali pia
kujenga jamii imara na ndio maana
tunalipa suala la elimu kipaumbelee kikubwa na leo
tumetembelea shule ya msingi Oysterbay, moja ya shule iliyopo maeneo
yetu ya biashara kwa ajili ya kuwapatia wanafunzi elimu ya kuwajengea uwezo wa
kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye safari yao ya kielimu na kutimiza
malengo na ndoto zao”.Alisema Tenga.
Alisema baadhi ya maofisa wa
TBL Group walipata fursa ya kuongea na wanafunzi wa darasa la sita wa shule hiyo na kuwapatia mafunzo mbalimbali
ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha na umuhimu za kuzingatia masomo yao
ili waweze kutimiza ndoto zao za baadaye katika maisha yao ya baadaye wakiwa ni
watoto wa kiafrika.
Tenga alisema mbali na
kuwapatia mafunzo kampuni imezindua shindano la wiki moja la kuandika insha ya
maneno 300 kwa wanafunzi hao kuhusiana
na changamoto zilizopo katika safari yao ya kielimu na jinsi ya kuzikabili
ambapo wanafunzi watatu wataoshinda watapata zawadi kutoka TBL .
Alisema mpango huu wa kukutana
na wanafunzi na kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo ni mpango endelevu ambao
utaendelea kutekelezwa na wafanyakazi wa kampuni wenye taaluma mbalimbali
katika maeneo yote ambako inaendeshea
biashara zake nchini pote.
Siku ya mtoto wa Afrika
huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na
umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu
ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika. Elimu
kwa watoto ndio imekuwa mada kuu kwa nchi nyingi katika kumuinua mtoto wa Afrika.







0 Comments