Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Miguu Wanawake (TWFA) Amina Karuma akifafanua jambo
Chama cha Mpira wa Miguu wanawake (TWFA), kimetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika Julai 8 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa (TWFA), George Mushumba
amesema kuwa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama
hicho zitaanza kutolewa Juni 19 huku mwisho wa kurudisha fomu hizo
ikiwa ni Juni 22.
Kamati hiyo imetoa ratiba ya kuelekea uchaguzi huo ambapo
Juni 23 mwaka huu kamati ya uchaguzi itapitia majina ya wagombea
walioomba nafasi mbalimbali.
Juni 24 kamati ya uchaguzi itatangaza majina ya wagombea
waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba au
kanuni za TWFA.
Pingamizi ya uchaguzi huo yatapokelewa kati ya Juni 26 na 27
mida ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na pingamizi yote kupitiwa
Juni 28.
Juni 29 kamati hiyo itatoa majumuisho ya pingamizi huku
tarehe 30 wagombea wote kufanyiwa usaili kabla ya mwezi Julai kutangaza
majina ya wagombea waliopitishwa
Kamati hiyo iliyo chini ya mwenye kiti huyo inatarajia
kupokea rufaa Julai 02, huku nafasi zitakazo gombewa katika uchaguzi huo
ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti, Katibu mkuu,
Katibu msaidizi, Mweka hazina, Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF pamoja na
wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

0 Comments