Na Jonas Kamaleki-MAELEZO
Zaidi ya vijana wapatao 1230 wametoa siri nzito kwa
Maaskofu na Mashekhe kutoka katika Kamati ya Kitaifa ya Maadili , Amani
na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini Nchini kufichua mtandao haramu
wa watu wanaoendesha mauaji na uhalifu mwingine kwenye mikoa
13, nchini kama njia muhimu ya kumpongeza IGP mpya, Saimoni Sirro.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Askofu William
Mwamalanga, siri hiyo imetolewa jana na vijana hao katika
siku ya tatu mkutano wa kujenga maadili kwa vijana unao fanyika Mbagala,
jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha vijana wa madhehebu
mbalimbali ya dini kutoka katika mikoa ya Pwani, Tanga, Lindi,
Morogoro,Dar es Salaam ambapo wameyataja maeneo ya Mkuranga, Rufiji
Kigamboni, Kibiti, Msata, Tanga mjini, Pemba na Unguja kuwa maeneo hatari
yanayowajengea vijana imani za kigaidi.
Aidha, Askofu Mwamalanga
alisema kuwa vijana 147 wa kiislamu wanaohudhuria mkutano huo wamewataja
baadhi ya watu ambao ni hatari na wamekuwa wakieneza
elimu ya mauaji kwenye misikiti mbali mbali nchini kwa kuiita Serikali
ya Awamu ya Tano jina la katili na kwamba elimu hiyo imesambazwa kwa kasi
katika mikoa ya Kagera, Tanga, Mwanza, Arusha, Pemba, Unguja, Dar es
Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro, Iringa, Singida, Dodoma, Pwani na Kigoma huku
vikosi vya vijana vikiandaliwa kufanya mauaji mara baada ya mufungo mtukufu
wa Ramadhani kama yale ambayo yamekuwa yakifanywa Mukuranga, Kibiti
na Rufiji.
Vijana hao wanamuomba IGP Sirro kuwachukulia
hatua kali maafisa wa jeshi hilo ambao wanatumia jeshi kupandikiza Umngiki,
na kwamba wana imani na IGP Sirro
amabaye kwa mujibu wa hao vijana hatamwangusha Rais Magufuli na
watanzania kwa ujumla.
Akifunga Mkutano huo Askofu Mwamalanga
amemtaja IGP Sirro kama polisi mahiri wa maadili na jemadali
mweledi wa mapambano hivyo amewataka vijana kote nchini kumuunga
mkono kwa kuwafichua polisi wote wanaoenzi uhalifu. “Tusipofanya hivyo tutakuwa
kama pipa zuri tunalo jaza maji wakati tukijua chini
limetoboka”,alisema Askofu Mwamalanga na kuongeza kuwa raia wema ni asilimia
99.9 wahalifu ni 0.1 hii ina maana kuwa ukiondoa polisi wahalifu
ndani ya jeshi hilo wahalifu ni wachache mno mitaani
watayeyuka wenyewe.
Aidha, Askofu huyo amewahimiza vijana na viongozi wa dini
kushiriki kwenye mafunzo hayo kote nchini ili wapewe ufahamu wa elimu ya
maadili ya kweli ili wawe walinzi wa taifa na kupenda amani na
kuweka uchu wa kuchukia rushwa na kujiwekea mitazamo ya kupenda kazi za baraka.
Kiongozi huyo wa dini amekemea vikali nyumba za ibada
kugeuzwa eneo la mafunzo ya uhalifu kwani ni aibu kwa msikiti au kanisa
kufanya mafunzo ya kigaidi ndani ya nyumba za
ibada kufanya hivyo ni ibada ya sanamu, watu wa jinsi hiyo hawana
uhusiano wowote na Mwenyenzi MUNGU ambaye kusudi lake ni kuondoa uovu kwa
mwanadamu.
Hivi karibuni yametokea mauaji ya viongozi wa Chama Tawala maeneo
ya Kibiti, Mukuranga na Rufiji na kufanya wakazi wa maeneo hayo kuishi kwa
wasiwasi na mashaka juu ya maisha yao. Wakati akiipishwa kuwa IGP, Kamanda
Simon Sirro alisema kupambana na kuondoa uhalifu kwa kushirikiana na raia wema
ni moja ya vipaumbele vyake.


0 Comments