Mwakilishi wa familia ya Bi Hasma Juma Jordan Jaddah akifuatilia
kwa umakini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu wakati akisisitiza juu ya taarifa iliyowasilishwa na
Mwenyekiti wa kamati ya Uchunguzi Dkt. Charles Majige juu ya kuibiwa
kwa mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akijibu maswali yaliyoulizwa na
Waandishi wa Habari juu ya tuhuma za kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi.Hasma
Juma katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. BaKari Kambi akitoa ufafanuzi
mbele ya waandishi wa habari (Hawapo kwenye picha) wakatati wa
uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi
Hasma Juma uliofanyika mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini
Dar Es Salaam.
Waandishi wa habari wa vituo tofauti wakifuatilia kwa umakini
uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za kuibiwa mtoto mmoja wa Bi Hasma
Juma uliowasilishwa leo na mwenyekiti wa kamati Dkt. Charles Majige
ambae pia ni Daktari bingwa wa Magonjwa yakina mama , uliofanyika leo
mapema katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
NA WAMJW DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa tume huru aliyoiunda ili kuchunguza malalamiko ya Bi. Asma Juma kuhusu kuibiwa mtoto mmoja kati ya mapacha wawili katika hospitali ya Rufaa ya Temeke Dar es salaam.
Akipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa tume hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama Dkt. Charles Majige Waziri Ummy amesema kuwa Bi. Asma Juma(29) hakuwa na watoto mapacha kama ilivyodaiwa na mlalamikaji huyo kutokana na kipimo cha Utra sound kukosea katika uchukuaji picha ya mtoto akiwa tumboni.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa tume huru niliyoiunda hivi karibuni na imethibitisha kuwa Bi. Asma Juma hakuwa na watoto mapacha ila uchukuaji mbaya wa picha ya mtoto aliyekuwa tumboni uliofanywa katika zahanati ya Huruma ukatoa matokeo hayo” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wanafamilia ya Bi. Asma wanatakiwa kumfariji ndugu yao na sio kumkumbushia jambo hili mara kwa mara kwani litamharibu kisaikolojia na kushindwa kutekeleza wajiu wake kwa mtoto kama mama mzazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Charles Majige Amesema kuwa Bi. Asma aliamini hivyo kwa sababu Hospitali ya temeke hawakumchukua vipimo vya picha bali walitumia taarifa ya vipimo vya awali .
Aidha Dkt. Majige Amesema kuwa tume hiyo imebaini kuwa Bi. Asma hakuibiwa mtoto na alikua hana mapacha kwa sababu uzito wake ulikua sio wa kubeba watoto wawili na katika chumba cha upasuaji kulikua na wataalamu 6 kutoka vitengo mbalimbali.
Kwa upande wake mwakilishi wa Familia ya Bi. Asma Juma ,Jordan Jaddah amesema kuwa anaishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kufatilia jambo hilo kwa ukaribu na kupata ukweli wa malalamiko yao na wameikubali taarifa hiyo .
“Tunaipongeza tume hiyo chini ya Wizara ya Afya na tunashukuru kwa msaada wao mwanzo mpaka mwisho na kutupatioa majibu ya kuridhisha nasi tutakuwa bega kwa bega katika kumfariji ndugu yetu kwa jambo hili lilitokea” alisema Bw. Jaddah.
Mbali na hayo Waziri Ummy amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa maagizo ya kila mtoto wa kike atakaepata ujauzito shuleni asirudi shuleni ila aendelee na masomo mengine ya ujuzi.




0 Comments