Katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )mkoani Pwani, dk.Zainab Gama ,akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Pwani, Mohammed Nyundo(MNEC)(picha na Mwamvua Mwinyi)
.......................................
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Zoezi
la uchukuaji fomu kugombea nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM)2017,mkoani Pwani,limeenda vizuri ambapo wanachama
wamejitokeza kwa wingi kuwania nafasi zilizotangazwa.
Zoezi
hilo lilianza rasmi july 2 na kukamilika july 10 na sasa hatua
inayosubiriwa itakuwa ni vikao vya mapendekezo kufanya kazi zake kwa
mujibu wa kanuni.
Katibu
wa CCM mkoani Pwani,Anastazia Amas alisema, waliochukua fomu kugombea
nafasi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa mkoani humo ni 11 na
nafasi ya mwenyekiti mkoa ni wanne.
"Wilaya
ya Bagamoyo waliojitokea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti
ni watatu,Kibaha Mjini ni 11,Kibaha Vijijini waliochukua fomu kwa
nafasi hiyo ni watano" alielezea.
Anastazia
alisema waliochukua fomu kuwania nafasi ya mwenyekiti wilaya ya Kibiti
ni watano,Kisarawe wanne,Mafia kumi,Mkuranga sita na Rufiji walichukua
fomu hiyo wanne.
KATIKA HATUA NYINGINE, katibu wa CCM Kibaha
Mjini,ABDALLAH MDIMU Mdimu ,alibainisha,nafasi ya katibu mwenezi
wamejitokeza watu watano,wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya kwa
makundi ya UVCCM,UWT na Wazazi wamejitokeza watu 36.
Katika ngazi ya mkutano mkuu wa Taifa 30,mkutano mkuu wa mkoa ni watu 26 na halmashauri kuu ya CCM ya mkoa wamejitokeza watu 13.
Mdimu alieleza kwasasa hakukuwa na harufu ya kubebana wala kupanga safu kutokana na elimu waliyoitoa kuanzia ngazi za chini.
"Tulitoa elimu ya kutosha na kusimamia zoezi zima ,mabadiliko ya CCM Mpya kiukweli yameonyesha kila jambo linawezekana "
"Hakujitokeza
hata mtu mmoja kuja na mbwembwe kufuata fomu hata kurudisha na hakuna
mtu ambae hajarudisha fomu ,zoezi limefanyika kwa kufuata demokrasia na
haki imetendeka kwani wengi wamejitokeza " alisema Mdimu .
WAKATI
HUO HUO,mwenyekiti wa jumuiya ya vijana (UVCCM)Mkoani Pwani ,MOHAMMED
NYUNDO(MNEC) ,alisema mchakato mzima upo vizuri na anaamini jumuiya hiyo
wilaya na mkoa itapata viongozi wenye uchungu na
jumuiya/chama,waadilifu,wachap akazi na wawajibikaji.
Alisema
wamekamilisha zoezi la utoaji na urudishaji wa fomu za kuomba kuteuliwa
kugombea nafasi mbali mbali ngazi ya mkoa na wilaya .
Nyundo
aliwashukuru vijana wote kwa kuitikia wito katika zoezi hilo muhimu la
mchakato wa kuwapata viongozi wa jumuiya na chama kwa muda wa miaka
mitano ijayo .
Alieleza wameridhishwa na idadi ya vijana waliojitokeza katika kuomba ridhaa katika nafasi zote.
"Ni
wajibu wetu kuhakikisha tunatenda haki katika nafasi zetu za kufanya
mapendekezo.;Tunaahidi kutenda haki,sisi tunaamini kila mmoja anayo haki
ya kuomba, kuchagua na kuchaguliwa." aliongeza Nyundo.
Nyundo
aliwasihi vijana wote, kama walivyokuwa watulivu wakati wa kuchukua
fomu, kujaza na kurejesha bila aina yoyote ya matendo ya kuvunja kanuni
za uchaguzi, basi wafanye hivyo hivyo katika wakati huu wa kusubiri
ratiba ya vikao vya maamuzi na kuelekea kwenye uchaguzi .
Anasema kipimo cha kwanza cha kiongozi bora ni uvumilivu, na hasa katika kipindi hiki.

0 Comments