Kaimu
Meneja wa Masoko na Huduma kwa Wateja, Bw. Cletus Mnzava (wa pili kulia)
akimfahamisha mwananchi aliyetembelea Banda la Wakala shughuli mbalimbali
zinazofanywa na kuratibiwa na Maabara zilizoko chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa
Serikali. Kushoto ni Mtumishi wa Wakala, Bw. Sabas Mandari, akisikiliza.
Kaimu
Meneja wa Maabara ya Kanda ya Mashariki, Bi. Everlight Matinga (wa pili kulia)
akimfahamisha mwananchi aliyetembelea Banda la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu
wa Serikali huduma zinazotolewa na Maabara za Wakala kuanzia Makao Makuu na
Kanda zake Sita zilizoko kwenye Mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dar es Salaam,
Mtwara na Dodoma.
Mkemia
Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele (kulia) akimsikiliza Afisa wa Polisi
aliyetembelea Banda la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuweza kufahamu
huduma mbalimbali zinazotolewa na Maabara zilizopo chini ya Ofisi yake kwenye
Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Saba Saba, Dar es Salaam.




0 Comments