Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,
Boniphace Butondo akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani la
kupokea na kujadili tarifa za kata za robo ya nne ya mwaka. Wengine pichani
kushoto ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri, Edward Shigela na Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri hiyo, Stephen Magoiga.
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao hicho. Wengine pichani
kuanzia kushoto ni Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Makamu mwenyekiti wa
halmshauri, Edward Shigela na Mwenyekiti Boniphace Butondo.
Madiwani na wataalamu kutoka halmashauri hiyo
wakifuatilia kikao hicho cha kupokea na kujadili tarifa za maendeleo ya kata.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack
Kangese akizungumza neno wakati wa kikao hicho.
Makamu mwenyekiti wa halmshauri, Edward Shigela
akizungumza wakati akifunga kikao hicho.
Madiwani na wataalamu kutoka halmashauri hiyo
wakifuatilia kikao hicho cha kupokea na kujadili tarifa za maendeleo ya kata.
................................
Na Robert Hokororo
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imepongezwa
kwa hatua yake ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi pamoja
na changamoto za uhaba wa fedha.
Pongezi hizo zimetolewa leo na mwenyekiti wa
halmashauri hiyo, Boniphace Butondo wakati akifungua kikao cha Baraza la
Madiwani kilichoketi kupokea taarifa za kata kwa kipindi cha robo ya nne ya
mwaka.
Butondo alisema miradi hiyo imetekelezwa kwa
kiwango kizuri pamoja na changamoto ya uhaba wa fedha iliyoikabili halmashauri
hiyo kwa kipindi hicho.
Alisema ushirikianoa baina ya madiwani na
wataalamu kutoka halmashauri hiyo ndiyo siri ya mafanikio hayo ambayo ni tija
kwa wananchi wanaowahudumia.
Aidha, aliwapongeza wataalamu hao kutoka idara
mbalimbali kwa kuwa na usimamizi mzuri ikiwemo wa fedha na maeneo ambayo miradi
hiyo inatekelezwa na kuwataka waendelee kushikamana.
“Naomba niwapongeze wote kwa ushirikiano mkubwa
mnaounesha najua kuna changamoto ya kuwa na mapato kidogo kutokana na hali ya
hewa na hivyo kuchangia kutopata pamba kwa wingi ambayo inaingiza mapato
halmashauri,” alisema.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya
lagana aliishukuru ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ushirikiano mkubwa kwa
halmashauri na hivyo kuchangia mafanikio hayo.
Tayari miradi mbalilimbali ya maendeleo ikiwemo
ujenzi wa vyumba vya madarasa, zahanati, barabara na maji imetekelezwa katika
kata mbalimbali za halmashauri ya wilaya hiyo.






0 Comments