Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika kilele cha Maadhimisho
ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
mjini Dodoma Julai 30, 2017.
Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa ikiongoza maandamano katika kilele cha
Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo
na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba (katikati) na Naibu Waziri wa Kilimomo,
Mifugo na Uvuvi, Tate William Ole- Nasha baada ya kuwasili kwenye ukumbi
wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma kuhutubia katika kilele cha
Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete mjini Dodoma Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Robert Mtitu
(kushoto) wa Chama cha Ushirika cha Wakulima cha Njombe wakati
alipotembelea banda la Ushirika huo katika kilele cha Maadhimisho ya
Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
mjini Dodoma Julai 30, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba.
Waziiri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sampuli mbalimbali za korosho
katika wakati alipotembelea banda la Ushirika wa Ruangwa, Nachingwea
Liwale Cooperative Union (RUNALI) Limited katika kilele cha
Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete mjini Dodoma Julai 30, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kushoto kwa Waziri ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Convenant, Sabetha Mwambenja.
.............
.............
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Serikali haitamsamehe mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhilifu wa mali za
fedha za Ushirika nchini.
“Kwa Serikali hii ya awamu ya
Tano tutachua hatua kali kwa wezi wa mali na fedha za ushirika na tunaendelea
kufanya usafi wa wabadhilifu hadi tupate viongozi waadilifu,”.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi,
Julai Mosi, 2017), katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD),
iliyoadhimishwa kitaifa mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Amesema miongoni mwa changamoto
zinazoukabili Ushirika nchini ni pamoja na wizi na ubadhilifu wa rasilimali za
Ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wasiokuwa waaminifu.
Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine ni baadhi
ya viongozi wa vyama vya Ushirika kutoheshimu miongozo ya vyama vyao na
kujifanyia mambo kwa maslahi yao binafsi.
Amesema katika kukabiliana na changamoto
hizo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake na kuweka mazingira rafiki ya
kustawisha Ushirika nchini ili kutoa fursa ya Ushirika kushamiri na kuwawezesha
Watanzania kumiliki uchumi wa nchi yao.
“Haikubaliki hata kidogo kuona sekta
hii inayosadifu maisha ya Mwafrika hamnufaishi ipasavyo , hivyo naelekeza Tume
ya Maendeleo ya Ushirika nchini ihakikishe kuwa vyama vya Ushirika vinaendeshwa
kisayansi na kwa mujibu wa sheria,” amesema.
Pia amezielekeza Kamati za Ushauri
za Mikoa na Wilaya nchini, ziingize agenda ya Maendeleo ya Ushirika kama moja ya
agenda muhimu inayopaswa kujadiliwa na kuwekewa maazimio ya utekelezaji. Pia
wawe na takwimu za vyama vya Ushirika na Wanaushirika.
Hata hivyo Waziri Mkuu amezielekeza
mamlaka zote zinazohusika na Ushirika nchini zijiwekee malengo yanayopimika ya
namna ya kuboresha sekta ya Ushirika.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameelekeza kwamba masuala yote
yanayohusu Ushirika wa kilimo nchini lazima yaratibiwe na Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi.
Aidha, Waziri Mkuu amezielekeza
Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zifanye mapitio
kubaini elimu na ujuzi katika ngazi zote za Ushirika kwa ajili ya kuwaandalia
kozi za muda mfupi za kuongeza ujuzi au kubainisha aina ya watumishi
wanaohitajika kwenye sekta hiyo.
Pia amewaagiza Maofisa Ushirika
nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri uchanguzi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
(AMCOS) na kuwaondoa wagombea wote waliowahi kuwa viongozi, ambao waliondolewa
madarakani kutokana na ubadhilifu wa mali na fedha za Ushirika.
Awali, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles
Tizeba alisema wizara itaendelea kusima na kuchukua hatua kwa viongozi wote wa
vyama vya Ushirika watakaobainika kufuja mali na fedha za Ushirika.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAMOSI, JULAI 1, 2017






0 Comments