Moja ya
vinara wa Teknolojia ya Habari na mawasiliano katika Maonyesho yanayoendelea ya
biashara jijiji Dar es Salaam – Multichoice Tanzania, imeendelea kutingisha
katika viwanja hivyo huku Makundi ya watu wakimiminika kupata ofa maalum ya
sabasaba kutoka DStv.
Multichoice
Tanzania (DStv) ambao walitangazwa rasmi kuwa washindi wa pili katika kundi la
washiriki wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wamemwaga ofa ya aina yake
ambapo gharama ya kufungiwa king’amuzi cha DStv pamoja na kifurushi cha mwezi
mzima ni shilingi 69,000 tu!
Akielezea
ofa hiyo Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria, amesema hii ni ofa
ya aina yake kwa wateja wa ving’amuzi kwani bei hiyo ni nafuu sana na ni maalum
katika msimu huu wa Sabasaba.
Amesema
Mteja mpya wa DStv sasa atapata king’amuzi cha DStv, kifurushi cha Bomba cha
mwezi mzima pamoja na ufundi bure kabisa! Ameongeza kuwa wameweka ofa hiyo kwa
viwango tofauti ili kumuwezesha mteja kuamua anachokipenda kwani amteja anaweza
kuamua kuchukua ofa ya king’amuzi kilichounganisha na kifurushi cha mwezi kwa
Shilingi 69,000 au hata kwa mwaka mzima kwa shilingi 300,000.
“Ofa
tulizonazo ni nyingi sana kwani pia tuna ofa ya ving’amuzi maalum vya kisasa
vijulikanavyo kama Explora vyenye uwezo wa kurekodi vipindi, kupeleka mbele au
kurudisha nyuma vipindi.” Alisema Alpha
Katika promosheni hii
mteja atakayelipa sh.185, 000 atapata king’amuzi maalum cha Explora na
kifurushi cha Compact mwezi mmoja wakati ambapo kwa sh.321,
mteja
atapata Explora, Smart LNB, Dish na Kifurushi cha Compact mwezi pamoja na
ufundi BUREE!
DStv ni
moja ya ving’amuzi maarufu hapa nchini ambavyo vimekuwepo kwa takriban miaka
ishirini na kujizolea umaarufu mkubwa hasa katika utoaji wa burudani, michezo,
habari za elimu, biashara, jamii, sayansi, teknolojia na utafiti.
Mwishoni
mwa mwaka jana, DStv ilipunguza sana gharama za vifurushi vyake ili kuwawezesha
watanzania wengi zaidi kufurahia huduma zao ambapo kwa sasa kifurushi maarufu
cha Bomba kinapatikana kwa Sh 19,975 tu!
Sambamba
na kupunguza bei, pia DStv ilianzisha chaneli maalum yenye maudhui ya
kitanzania ijulikanayo kama Maisha Magic Bongo DStv namba 160. Chaneli hii
imejipatia umaarufu mkubwa sana kwani imekuwa ikirusha maudhui ya Kitanzania
ikiwemo muziki, michezo ya kuigiza, filamu na tamthilia za hapa nyumbani
ikiwemo tamthilia ya HUBA ambayo kwa sasa inaongoza kwa umaarufu hapa Afrika
Mashariki.




0 Comments