Mhariri Mtendaji wa
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz akielezea jambo wakati wa
mkutano wa majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Mtandao leo
Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu
kuhusu masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Tanzania na Wizara ya Habari, na masuala ya Mitandao China.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia James Wambura na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –
MAELEZO, Bw. Rodney Thadeus.
Naibu Waziri wa
Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza
wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya
Mtandao leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la
kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania na Wizara ya Habari, na masuala
ya Mitandao China. Kutoka kulia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya
Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –
MAELEZO, Bw. Rodney Thadeus (katikati).
Naibu Waziri wa
Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akifurahia
jambo akiwa pamoja na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)
Dkt. Jim Yonaz (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO,
Bw. Rodney Thadeus (kushoto) alipokuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mkutano wa
majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Mtandao leo Jijini Dar
es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu
masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo ya Tanzania na Wizara ya Habari, na masuala ya Mitandao China.
(Picha na: MAELEZO)
.......................
Na.
Bushiri Matenda-MAELEZO
Serikali
imesisisitiza kuwa matumizi ya mitandao lazima yazingatie sheria zilizopo na
kuheshimu maadili, utamaduni na ustaarabu wa watumiaji.
Hayo yameelezwa jana
na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alipokuwa
akifunga mkutano juu ya njia mpya za mawasiliano ulioandaliwa na Serikali ya
Tanzania na China uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu
Nyerere Jijini Dar es Salaama.
“Matumizi ya mitandao
ni lazima yasimamiwe, yaratibiwe na yafanyike kwa mujibu wa sheria ili mitandao
iweze kuendelea na kuimarika chini ya utawala wa sheria,” amesema Wambura.
Aliongeza kuwa katika
hali ya sasa ya matumizi ya mitandao ni lazima juhudi zaidi ziongezwe katika
kuimarisha maadili na kuhimiza ustaarabu na msisitizo zaidi uwekwe katika
ufundishaji wa maadili katika matumizi ya intaneti ili kusaidia kukua zaidi kwa
mitandao katika hali salama na yenye maadili.
Wambura aliwaambia washiriki
wa mkutano huo kuwa, Serikali ya Tanzania inayapa uzito mkubwa maendeleo ya
intaneti, kwa kuwa intaneti ni moja ya njia muhimu katika kusaidia kuinua hali
za maisha ya wananchi wake kupitia matumizi ya teknolojia ya habari na
mawasiliano.
“Tangu mwaka 1995
ambapo Tanzania iliunganishwa na huduma za intaneti, tumekuwa tukichukua hatua
kuhakikisha matumizi sahihi ya huduma hiyo ambapo tumetunga sheria na mfumo wa
usimamizi na usalama wake, pia tunaendelea kuimarisha miundombinu ya teknolojia
ya habari na mawasilino pamoja na kufanya maisha ya wananchi wetu kuwa mazuri
zaidi kupitia matumizi ya teknolojia hiyo” alibainisha Wambura.
Aidha Wambura alieleza
kuwa kila siku Dunia inashuhudia kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia ya
habari kupitia intaneti ambayo yameifanya Dunia kuwa kijiji na kurahisisha
mawasiliano ambapo watu wanawasiliana
kwa urahisi wakati wote bila vizuizi.
Alisema kuwa upo
umuhimu kwa Serikali hizo mbili kuweka
mazingira wezeshi kisheria na uratibu utakaoweza kuhamasisha ukuaji wa matumizi
ya teknolojia ya habari na mawasiliano na kuvutia ubunifu kwa kizazi cha sasa.
“Ushirikiano unaozingatia
haki, usawa na kuaminiana ni kitu kisichoepukika ikiwa Dunia inataka kuwa na
mtandao salama na wenye manufaa kwa wote,” alifafanua Wambura.
Mkutano huo umehudhuriwa
na wadau wa habari kutoka Tanzania na China ambapo uliongozwa na kauli mbiu ya
“Maendeleo ya vyombo vya habari yanayochochewa na ubunifu.



0 Comments