Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza katika Mkutano wa Wajasiriamali Wilaya ya Mkuranga juu ya kujiwezesha kiuchumi kutokana na ardhi walio nayo.
Mkurugenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza na wanawake wajasirimali wa Mkuranga juu fursa zilizopo katika Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkurnga, Abdallah Ulega akizungumza na wanawake wa Wilaya hiyo juu kutumia maada za mkutano katika kuzifanya fursa.
Mkurugenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde (wa kwanza kulia )akisalimiana na Mwenyekiti wa Jukwa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga, Mariam Abdallah, katika Mkutano wa Wajasiriamali mkoani Pwani.
Sehemu ya Jukwa la wanawake walikuwapo katika mkutano huo ulifanyika Mkuranga.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga
amewatahadharisha wananchi wa wilaya hiyo kuacha kuuza ardhi hovyo na badala yake kuyatumia maeneo
hayo katika kufanya shughuli za uchumi.
Mkuu wa Wilaya aliyasema wakati wa Mkutano wa Wanawake 402 Jukwaa Wanawake wa Wilaya ya
Mkuranga ulioandaliwa na Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji Kiuchumi , amesema
kuwa wananchi wa Mkuranga wakiitumia ardhi vizuri itawapa maendeleo na sio
kuuza na kwa ajili ya kucheza ngoma.
Amesema Mkuranga ina ardhi ya kutosha
yenye rutuba lakini wananchi wanashindwa kuitumia katika kujiletea maendeleo na kufanya kuwa na maisha magumu ya kujiendeesha kiuchumi.
Aidha amesema mkutano wa wanawake wajasiriamali uwe chachu
katika kuanza kuitumia ardhi katika shughuli za kilimo na mazao watayoyalima watapata masoko.
Nae Balozi wa Heshima wa Sheli sheli,
Maria Paul amesema kuwa wanawake walime matunda Passion na Nanasi na kuweza
kuyanunua mwenyewe hivyo hawatakuwa na usumbufu wa soko kwa matunda hayo.
Maria amesema kuwa wananchi wa
Mkuranga wamepata bahati ya ardhi lakini ardhi hiyo haitumiki katika kuwapa
maendeleo wakiwemo wanawake wa wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wajasiriamali
Wilaya ya Mkuranga, Mariam Abdallah amesema wakati wa maendeleo umefika
wakutumia ardhi katika kuwaletea maendeleo.
Kwa Upande wa Mbunge wa Mkuranga,
Abdallah Ulega amesema kuwa kuna maendeleo yamewafikia wananchi iliyokuwa changamoto ikiwemo maji ambapo visima nane vimechimbwa katika
vijiji vya Kimazichana Magharibi, Mkerezange, Midimuni,Ngole , Mwanambaya ,Yava
yava pamoja na Mlaleni.
Aidha Mbunge ameomba kwa Mkuu wa
Wilaya kutumika kwa Kituo cha Mti Pesa kwa abiri kushuka na kupanda ikiwa na biashara katika mida jioni ambapo
Mkuu wa Wilaya alikubali na kusema jumatatu kituo hicho kitatumika.
Amesema kuwa vijiji vyote vitapata
umeme katika mradi umeme vijiji awamu ya tatu na upande barabara ya lami kutoka
Mkuranga Mjini kwenda Hospitali ya Wilaya Kupitia ofisi ya Mkuu wa
Wilaya hadi Halmashauri.
Ulega
ameomba barabara Vikindu Viazi hadi Marogoro, Sangatini pmoaja na
Barabara ya Kiguza , Hoyoyo , Kitonga kuingia katika barabara za Mkoa ili
kutokana na fursa za maendeleo ya maeneo hayo.
0 Comments