Andy Murray na Johanna Konta
watapambana kuhakikisha kuwa wanafika robo fainali ya michuano ya
Wimbledon ya wanaume na wanawake itakayochezwa siku ya leo.
Kama watafanikiwa itakuwa ndio kwa mara ya kwanza Uingereza kufanya hivyo tokea mwaka 1973.
Konta atapambana na Caroline Garcia katika mchezo wa ufunguzi.
Bingwa mtetezi Murray yeye atacheza na Benoit Paire siku hiyo ya Jumatatu.
Roger
Federer, Novak Djokovic, Rafael Nadal na Murray kwa pamoja wameshinda
vikombe 14 vya Wimbledon, huku mshindi mara tano Venus Williams akiwa
ndiye pekee aliyeng'ara kwa upande wa kinadada.

0 Comments