Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala limefanya oparesheni maalum maeneo ya Posta ya Zamani jirani na kituo cha Mwendokasi katika ukuta wa uzio wa bandari na kufanikiwa kuwakamata vijana kumi na kuchoma vibanda vyao walivyokuwa wanavitumia kwa matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya.
Akizungumza na Mwandishi wa MCL (Moshi Shabani) aliyekuwepo eneo la tukio kamanda ambaye aliyeomba jina lake kutochapishwa na chombo chetu cha habari, ameeleza kuwa wameamua kufanya oparesheni hiyo ya kushtukiza ili kukabiliana na vijana ambao wamezoea kufanya biashara na kutumia dawa za kulevya kinyume cha taratibu na sheria za nchi.
Pia ameuomba uongozi wa bandari kushirikiana nao kuhakikisha wanaziba njia ya kwenye uzio wa bandari ambao vijana hao hutumia na kujificha katika vibanda ambapo hufanya biashara hiyo haramu.
Kwa upande wake Mkazi wa Jijini Dar es Salaam Praygod Thadei amelipongeza jeshi la polisi kwa hatua hizo madhubuti kwani eneo hilo lilikuwa linatishia amani majira ya usiku hivyo wanaimani kwa hatua zinazo chukuliwa na jeshi la polisi eneo hilo litakuwa salama.
Chini matukio mbalimbali ya Oparesheni hiyo.












0 Comments