Wayne Rooney (wa tatu
kushoto) kushoto akiwa na wachezaji wenzake walipokuwa Jijini Dar es Salaam
ambapo timu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki
ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
..........................................................
Na.
Mwandishi Wetu-MAELEZO
Timu ya Soka ya Everton
inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza imemaliza ziara yake ya siku mbili
nchini Tanzania na kuelezwa kufurahishwa na namna Watanzania walivyoipokea timu
hiyo.
Timu ya Everton iliwasili
Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo jana ilicheza mchezo wa kirafiki
dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.
“Imekuwa ni uzoefu mpya
kwangu kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini sasa Makamu wa Rais atakuwa
akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney kupitia tovuti ya timu hiyo.
Pia katika akaunti yake ya
mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru washabikji wa Tanzania kwa kuiunga
mkono Everton katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka
Kenya.
“Great start to the pre-season. Special
thanks to the fans supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney akitoa shukrani
za pekee kwa washabiki wa Tanzania.
Kwa upande wa Kocha wa
timu hiyo, Ronald Koeman alielezea kufarahia ziara ya kuja Tanzania na zaidi ni
kutokana na hali ya urafiki iliyooneshwa na washabiki wa soka nchini.
Rooney pia aliungana na wachezaji
wengine kama Morgan
Schneiderlin, Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas
wa
timu hiyo walipata fursa ya kujifunza tamaduni za kimsai, kujifunza kupika
chakula cha asili, kutembelea shule yenye wanafunzi wenye mahutaji maalum na
pia kufanya mazoezi na timu ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (Albino United).
Timu ya soka ya Everton
ilifanya ziara nchni Tanzania ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor
Mahia ya Kenya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye
alikuwa Mgeni Rasmi, Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wageni mbalimbali
kutoka ndani na nche ya nchi.

0 Comments