Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisikiliza maelezo ya kimondo
kilichopo Mkoani Songwe wakati wa ziara yake Mkoani hapo.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akiongea na
Menejmenti ya Halmashauri ya Mkoa wa Songwe (Hawapo pichani) alipotembelea mkoa
huo jana , kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Bw. Herman Paul
Tesha.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole akiangalia moja ya kazi za
filamu iliyoandaliwa na wasanii wa Mkoa wa Songwe alipotembelea mkoa huo jana,
Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Herman Paul Tesha
Wazee wa kimila kutoka koo mbalimbali
za Mkoani Songwe walipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(hayupo katika
picha) jana mkoani hapo.
......................
Na Zawadi Msalla-WHUSM
Watumishi wa Mkoa wa Songwe wameshauriwa kuwa na utamduni wa
kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni nyenzo muhimu ya kufikia malengo na azma
iliyowekwa na Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi
ya Viwanda.
Hayo yamezungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati alipokutana na
Sekretarieti ya Mkoa huo,na kuwaeleza kuwa ni wakati muafaka kwa
watumishi kupata na kutoa elimu sahihi ya kuwafanya wananchi wapende
utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii bila kulazimishwa.
” Ni vizuri watumishi wakawa na elimu ya kutosha kuhusu utamaduni
wa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya kiutumishi ili kuweza
kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi yetu”
alisema Prof.Gabriel
Prof. Elisante aliongeza kuwa ni muhimu kwa watumishi
wa Umma na watanzania kwa ujumla kufanya kazi kwa kushirikiana
ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa manufaa ya taifa .
Aidha alieleza kuwa ni budi Watanzania kufuata maadili na
kuzingatia muda katika utunzaji wa rasilimali za nchi kwa manufaa
ya kizazi kilichopo na kijacho kwa kuwa ni vigumu kutegemea mtu kutoka nje ya
nchi kutunza rasilimali za nchi yetu.
Vilevile Katibu Mkuu Prof.Elisante aliwaomba watumishi wa
Sekretarieti ya Mkoa wa Songwe kuunga mkono jitihada za Rais John Pombe
Magufuli za kuipeleka mbele nchi katika uchumi wa kati na kuwa Tanzania ya
Viwanda.
Mbali na hayo Prof.Elisante aliipongeza Wilaya ya Ileje kwa kuwa
mfano katika utendaji uliopelekea mafanikio makubwa kwa mkoa wa Songwe na
kuzitaka Wilaya nyingine kuiga mfano huo.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa Bw.Herman Tesha aliahidi kutekeleza
ushauri ulitolewa na Katibu Mkuu Prof.Elisante licha ya uchanga wa mkoa wake
kwa kuwa anaamini mwamko na ari ya watumishi waliopo kwa pamoja wanaweza
kuleta maendeleo.




0 Comments