Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Magereza na Mfuko wa pensheni wa
PPF baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya
kutembelea kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi pamoja na kuangalia maendeleo
ya ujenzi wa kiwanda kipya eneo la Karanga Moshi Mkoani Kilimajaro.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira alipofika katika eneo
la mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi kilichopo Karanga
Moshi Mkoani Kilimajaro kinachoendeshwa kwa ushirikiano kati ya PPF na Jeshi la
Magereza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango wakiangalia moja ya jozi ya kiatu kilichotegenezwa
na kiwanda cha Karanga ambacho kinafanyiwa marekebisho ili kuongeza uzalishaji,
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama(wapili kutoka
kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango(watatu kutoka kushoto),
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda na
Mkuu(wakwanza kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.
Mhandisi Hamad Masauni(wanne kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Mama Anna
Mghwira wakiangalia moja ya jozi ya kiatu kilichotegenezwa na kiwanda cha
Karanga Kilichopo mkoani Kilimanjaro kinachoendeshwa kwa ushirikiano kati ya
PPF na Jeshi la Magereza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni za wastaafu
PPF, Bw.William Erio akitolea
maelezo kuhusu mipango ya ujenzi wa kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi ambapo
alisema kiwanda hicho kitagharimu bilioni 54.4 na kitakuwa na uwezo kuzalisha
futi mraba za ngozi milioni tatu laki saba na nusu kwa mwaka pamoja na
kuzalisha viatu vya kijeshi na kiraia jozi milioni moja na laki mbili kwa
mwaka, pamoja na kutoa soli laki tisa kwa mwaka pamoja na kutoa bidhaa nyingine
za ngozi kama mikanda,mabegi na mikoba ya akina mama takribani elfu arobaini na
nane kwa mwaka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipimwa mguu ili
kutegenezewa kiatu alipofanya ziara katika eneo la mradi wa uboreshaji na
ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha Karanga Moshi Mkoani
Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda na Mkuu, Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni, na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro
Mama Anna Mghwira wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa PPF na
Jeshi la Magereza baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi
pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kipya eneo la Karanga Moshi
Mkoani Kilimajaro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira
na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiongea baada ya ziara ya ya
kutembelea kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi pamoja na kuangalia maendeleo
ya ujenzi wa kiwanda kipya eneo la Karanga Moshi Mkoani Kilimajaro ambapo
aliipongeza PPF pamoja na Jeshi la Magereza kwakufanya maamuzi sahihi
yanayoendana na dira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati
kupitia viwanda kwa kuja na mradi wa uboreshaji na ujenzi wa kiwanda kipya cha
kuzalisha bidhaa za ngozi cha Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Picha na: MAELEZO
..............................
Na: Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira
na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza bodi ya wadhamini ya
Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa uamuzi wa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika
kujenga kiwanda kipya pamoja na kuendeleza kiwanda cha Bidhaa za ngozi Karanga
Kilichopo Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea na kuona
maendeleo ya kiwanda hicho Waziri Mhagama amesema kuwa PPF na Jeshi la Magereza
wamefanya maamuzi sahihi yanayoendana na dira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda.
“Dhamira ya Serikali ni kufikia uchumi wa kati
kupitia viwanda, PPF na Jeshi la Magereza mmeonesha mfano, uboreshaji wa
kiwanda hiki na ujenzi wa kiwanda kingine ambacho kitakuwa na viwanda
vidogovidogo vinne ni ishara ya kutimia kwa ahadi ya Rais wetu Dkt. John
Magufuli ya kuwa na uchumi wa kati kupitia Viwanda”. Alisema Mhe. Jenista.
Aidha, alisema kuwa lengo la Serikali ni
kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha na Serikali
itatoa msaada popote inapohitajika ili kwa haraka nchi yetu ianze kuzalisha
viatu ambavyo vitauzwa nje ndani na nje ya nchi hatimaye kuliingizia taifa
mapato.
Akizungumzia kuhusu ajira zitakazozalishwa na
kiwanda hicho Waziri Mhagama amesema kuwa kiwanda hiki pekee kitatoa ajira za
moja kwa moja 689 na zisizo za moja kwa moja 1800 hivyo kusaidia kukabiliana na
changamoto ya ajira hasa kwa vijana nchini.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
amesema kuwa PPF na Jeshi la Magereza lazima wahakikishe mipango waliyoiweka ya
ujenzi wa kiwanda kipya na maboresho ya kiwanda cha zamani yanafanyika kwa
wakati ili kwa haraka uzalishaji uanze na hatimaye nchi iweze kunufaika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi
Hamad Masauni ameishauri mifuko mingine ya pesheni kutumia fursa zilizopo Jeshi
la Magereza ikiwamo maeneo na rasilimali watu katika kufikia azama ya serikali
ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda.
Akiongelea ujenzi wa kiwanda kipya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni za wastaafu PPF, Bw.William
Erio amesema kuwa kiwanda hicho kitagharimu shilingi bilioni 54.4 na kitakuwa
na uwezo wa kuzalisha na wanategemea kuzalisha futi mraba za ngozi Milioni tatu
laki saba na nusu (3,750,000/=) kwa mwaka.
Vilevile Bw. Erio amesema
kuwa kiwanda hicho kitazalisha viatu vya kijeshi na kiraia jozi milioni moja na
laki mbili kwa mwaka, pamoja na kutoa soli laki tisa kwa mwaka pamoja na kutoa
bidhaa nyingine za ngozi kama mikanda,mabegi na mikoba ya akina mama takribani
elfu arobaini na nane kwa mwaka.








0 Comments