Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa
akizungumza na washiriki wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo mapema hii leo katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu toka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Simon Msanjila (kushoto) akitoa neno la utangulizi kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa
maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Vyuo Vikuu nchini Prof. Jacob Mtabaji (kushoto)
akitoa neno la utangulizi kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu
nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelekezo toka kwa mshiriki toka Chuo Kikuu
Mzumbe wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelekezo toka kwa mshiriki toka
Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini
mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelekezo toka kwa mshiriki toka
Chuo Kikuu Nelson Mandela wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu
nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelekezo ya namna
ya kujiunga na vyuo vikuu wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu
nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
..................................
Na. Paschal Dotto - MAELEZO
Vyuo vikuu vilivyofungiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo
2017/2018 vimetakiwa kukamilisha matakwa yanayohitajika kwa kufuata taratibu zilizowekwa
na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa leo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 12 ya vyuo vikuu
nchini yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini, Dar es Salaam.
“Vyuo vikuu vyote nchini vinatakiwa kutoa elimu bora kwa wahitimu
ili kuwawezesha kujiajiri na kuendana na Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kujenga Tanzania yenye viwanda,” amesema Majaliwa.
Majaliwa ameongeza kuwa, ili kujenga uchumi wa viwanda vyuo vikuu
hapa nchini vinatakiwa kufundisha na kuwawezesha wahitimu kujiajiri ili
kuendana na ushindani katika soko la ajira kitaifa, kimataifa na Dunia kwa
ujumla.
Vile vile vinatakiwa kukuza stadi katika sekta ya viwanda kwa
kupata wasomi waliofundishwa kwa vitendo kutoka katika vyuo mbalimbali, kuweka
mikakati na kuboresha elimu ili kuendana na dhamira ya Serikali pamoja na
kuweka mitaala mizuri kwa wanafunzi katika vyuo hivyo ili kuendana na
mabadiliko yaliyofanywa katika udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo
2017/2018.
Aidha Majaliwa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa bajeti Shilingi Tril. 4.7 kwa Wizara
ya Elimu ili kuboresha elimu ambayo itahusisha katika kujenga na kuboresha
miundombinu ya elimu hapa nchini ikiwemo mikopo ya elimu ya juu na mahitaji
mengine ya vitabu kwa shule za Sekondari.
Naye Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage
amevitaka vyuo vikuu hususani vile vilivyofungiwa kwa kutokidhi matakwa ya
utoaji elimu hapa nchini, kukaa na kuweka mambo sawa ili waweze kufanyiwa
uhakiki upya na TCU.
“Ili chuo kiweze kukamilika kutoa elimu bora lazima kiwe na
miundombinu bora, wahadhili waliobobea, mitaala safi, wanafunzi wenye sifa na
kujituma,” amefafanua Mwijage.
Maonesho hayo ni ya 12 tangu yalivyoanzishwa mwaka 2005 ambapo kwa
mwaka huu zaidi ya vyuo vikuu 80 kutoka ndani na nje ya nchi vinashiriki.
Maonesho yatafanyika kwa siku Nne kuanzia Julai 26 hadi Julai 29 mwaka huu.







0 Comments