Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua
risiti ya mmoja wa mama aliyefika kwenye
hospitali ya Wilaya ya Chato aliyekuwa amemleta mtoto wake kupata
matibabu.Mhe.Waziri alikua akijiridhisha kama mama huyo amelipishwa fedha
katika matibabu ya mtoto kwakuwa
matibabu kwa mtoto chini ya miaka mitato huduma hutolewa bila malipo
Waziri Ummy akikagua duka la dawa lililopo
kwenye hospitali hiyo (Duka la MSD) ambalo linasaidia upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo pamoja na vituo vya
afya pamoja na zahanati za jirani.Kulia mwisho ni Mbunge wa Jimbo la Chato na
naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani
Waziri wa Afya akitoka kutembelea Wodi ya Wazazi
iliyopo kwenye Hospitali hiyo,kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Athanasi
Ngambakub na katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na madini Dkt.Medard Kalemani
Waziri Ummy wakijadiliana jambo kwenye jengo jipya
linalojengwa la upasuaji,ambapo Waziri ameagiza jengo hilo likikamilika wawape
kipaumbele akina mama wajawazito ili kuweza kuokoa vifo vitokanavyo na uzazi.
Katika wodi waliyolazwa watoto Waziri Ummy
akimsalimia mmoja wa mtoto aliyelazwa hospitalini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga akimsisitiza jambo Waziri wa Afya wakati wa kuongea na watumishi
wa hospitali hiyo,kushoto ni Mkuu wa Wilaya Mhe.Shabani Ntalambe
Dkt.Kalemani akizungumza na watumishi wa
hospitali hiyo(hawapo pichani) mara baada ya kutembelea hospitali hiyo
Meneja wa Kanda ya Mwanza wa Bohari Kuu ya Dawa
(MSD) Victory Sungusia akijibu swali toka kwa Waziri Ummy wakati wa kuongea na
watumishi wa hospitali ya Wilaya ya Chato
Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo
wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(hayupo
pichani)
Picha ya pamoja ya Mawaziri,Viongozi wa Mkoa na
Wilaya pamoja na baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo mara baada ya kumaliza
ziara (Picha zote na Wizara ya Afya)










0 Comments