Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wilayani humo. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo.
Makamu Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Bw. Mohamed Dadi (kushoto) akionesha maendeleo ya Skimu hiyo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo walipotembelea Skimu hiyo.
Kaimu Afisa Tarafa ya Mang’ula, Bw. Omary Said (kulia) akitoa maelezo kuhusu Mradi wa Kilimo Shadidi kinachofanyika katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kushoto) na Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati). Wengine wanaosikiliza na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo.
Maafisa kutoka Benki ya Kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakingalia Mpunga uliyo tayari kuvunwa katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa.
Meneja Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Bw. Dickson Pangamwawe (wapili kushoto) akionesha maendeleo ya ukuaji wa miwa ya Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa ambao ni wanufaika wa mikopo ya Benki ya Kilimo. Wanaotazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege.
Wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa wakipanda mpunga kwa kutumia njia ya kilimo shadidi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege (kushoto) akiongea na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ulioambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kulia). Benki ya Kilimo ilifanya ya ukaguzi wa miradi iliyopatiwa mikopo ili kujionea maendeleo ya miradi wilayani Kilombero.
Katika kuhakikisha miradi inayopatiwa mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), uongozi wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,Bw. James Ihunyo wametembelea miradi minne iliyopo wilayani humo.
Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula. Nyingine ni Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema ameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo hali inayochochea ari ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha wakulima nchini.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo aliwaasa wakulima hao kurudisha mikopo kwa wakati ili wakulima wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.
“Lengo la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,” Bw. Ihunyo alisema.
Zaidi ya Shilingi bilioni 2 imekopeshwa kwa wakulima wa mpunga na miwa wilayani Kilombero.
0 Comments