Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akifungua kikao
kazi cha wadau (hawapo pichani) waliokuta kutathmini Sera ya Maendeleo ya
Wanawake na Jinsia kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la Wizara Magogoni
Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017 kulia ni Mkurugenzi wa Mashirika yasiyokuwa ya
Kiserikali Bw. Marcel Katemba (kulia) na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi (aliyesimama)
akibainisha malengo ya kikao cha wadau (hawapo pichani) wanaokutana kutathmini
Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia katika ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara
ulioko Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017 Kulia ni Katibu Mkuu
Sihaba Nkinga.
Mtaalam mwelekezi anayeongoza kazi ya kutathmini Sera ya Maendeleo ya Wanawake
na Jinsia Prof. Linah Mhando, akiwasilisha rasimu ya awali ya taarifa ya
mapitio ya Sera hiyo katika kikao cha wadau (hawapo pichani) kinachofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ulioko Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9
Agosti, 2017.
Baadhi ya wadau wanaoshiriki kikao kazi cha kutathmini Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kutoka taasisi mbalimbali wakifuatilia mada mbaimbali katika kikao kinachofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ulioko Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017.
Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
.................
Na
Erasto Ching’oro- WAMJW
Katika
kuhakikisha Taifa linakuwa na Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ambayo ni
shirikishi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeandaa kikao kazi kwa ajili ya kukusanya maoni zaidi yatakayosaidia kuhuisha
sera hiyo.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga mara baada ya kikao
na wadau kutoka taasisi mbalimbali katika mwendelezo wa mchakato wa ukusanyaji
wa maoni ya ambayo yatasaidia kubaini mapungufu, na changamoto zilizopo katika
Sera iliyopo na hivyo kusaidia uboreshaji wa Sera hiyo kwa kuzingatia mahitaji
ya kijinsia kwa ajili ya maendeleo ya wanawake, wanaume, wavulana wasichana na
watoto.
“Sera
iliyopo ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 imechukua muda mrefu
kufanyiwa tahmini kutokana na ukweli kuwa zoezi la tathmini linahitaji muda wa
kutosha sanjari na uhakikika wa upatikanaji wa rasimali fedha kufanikisha kazi
hii” alisema Bibi Sihaba.
Kwa
upande wake Msauri Mwelekezi Profesa Linda Muhando aliipongeza Wizara kwa
kuridhia mchakato wa kutathmini sera hiyo na kujumuisha wadau hatua amabyo
itasaidia kupata mchango wa wananchi wengi zaidi na kuwezesha kupata masuala
mapya amabyo hayako kwenye sera hiyo na kuyajumuisha katika rasimu ya sera
inayofanyiwa mapitio.
Kikao
kazi cha tathmini ya Sera hiyo kinatoa fursa kwa wadau kuibua changamoto,
mapungufu yaliyopo na kuimarisha uzingatiaji wa mahitaji ya wanawake na wanaume
ili kutoa fursa sawa ya upatikani haki na usawa kwa watu wote.
Maandalizi
ya uboreshaji wa Sera hii utajumuisha usambazaji wa sera kwa wananchi, kutoa
elimu kwa umma ili kufahamu mwongozo wa kisera, na kuiweka katika lugha nyepesi
ili kujenga ufahamu wa wananchi katika wigo mpana zaidi. Aidha, ukusanyaji wa
maoni ya wadau utasaidia kupanua ushirikishaji wa wananchi katika kuandaa sera
na kufanikisha utekelezaji wake kwa kuzingatia wakati.






0 Comments