Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Ufyemba kata ya Wasa wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa katika
jitihda za kuhamasisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick
Golwike akihamasisha wananchi kuendeleza ari ya kushiriki kazi za maendeleo ya
kijiji chao cha Ufyemba mkoani Iringa kwa kushirikiujenzia wa zahanati hiyo ambayo unajengwa na wananchi wa
kijiji hicho kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe ili kusogeza huduma za afaya
kijijini.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinda akishirikiana na wakazi wa Kijiji
cha ufyemba kubeba matofali katika kufanikisha ujenzi wa Zahanati kijiji cha
Ufyemba kata ay wasa, iliyoko wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.
Wananchi wa kijiji cha Ufyemba wakishiriki
katika kubeba matofali na kujenga jingo la zahanati ya kijiji hicho ili kuondokana
na taatizo la kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.
Wananchi wa kijiji cha Ufyemba wakimsikilizakwa
makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi.
Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati akiwahamasisha kujitolea katika kuibua, kupanga
na kutekeleza shughuli za maendeleo katika Kijiji chao.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi mifuko 50 ya saruji
kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Ronaganius Lunyungu ili kuunga mkono
jitihada za wananchi hao katika kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha
Ufyemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi pesa kwa Mwenyekiti
wa Kijij cha Ufyemba Bw Roganius Lunyungu zilizopatikana katika harambee ili isaidie katika kumalizia Ujenzi wa
zahanati ya kijiji cha Ufyemba.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Ufyemba
wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kushiki kwa
vitendo kazi za miradi ya maendeleo iliyoibuliwa na kutekelezwa kwa kutumia
nguvu za wananachi wenyewe katika kijiji hicho.
Picha na Erasto Chin’goro WAMJW IRINGA










0 Comments