Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Mbunge
wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka amesali kanisa la KKKT Tumbi
ambapo pamoja na mambo mengine amechangia 3,000,000/- kwenye ujenzi wa
mradi wa wanawake wa KKKT kanisani hapo.
Aliwataka wanawake ,vijana kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kujikwamua kiuchumi .
Mapema
akitoa salamu za waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba
ambaye alitakiwa awe Mgeni Rasmi katika siku hii lakini hakufika kwa
sababu ya majukumu mengine, Mbunge Koka aliwasilisha 6,000,000/- mchango
wa mhe waziri kwenye miradi hiyo ya akinamama wa KKKT .
Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka ,mwenye suti nyeusi
akiwa katika picha ya pamoja baada ya misa kwenye kanisa la KKKT Tumbi
Kibaha.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)


0 Comments