Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo akizungumza leo
wakati alipokabidhiwa mradi wa Maboresho ya Mtaa Samora jijini Dar es
salaam na Shirika la Maendeleo la Serikali ya Japan (JICA)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya
Ilala Sophia Mjema wakikata utepe leo wakati wa makabidhiano ya mradi
wa Maboresho ya Mtaa Samora.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjemna Meya wa Jiji la
Dar es salaam Isaya Mwita wakiongozana wakati wa makabidhiano ya mradi
wa Maboresho ya Mtaa Samor.
………………………………………………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda leo amekabidhiwa mradi wa Maboresho ya Mtaa Samora jijini
Dar es salaam uliogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 840
zilizofadhidhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la
maendeleo Japan (JAICA) na Manispaa ya Ilaa uliokamilika kwa 100%.
Mradi huo umehusisha ujenzi wa sehemu za Maegesho, mapumziko
ya watu,upandaji wa miti na Maua,maboresho ya mazingira,uwekaji wa alama
za barabarani pamoja na maboresho ya mitaa kuanzia Makutano ya Barabara
ya Samora na Morogoro ikienda sambamba na kupunguza msongamano.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Makonda amemuagiza Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuhakikisha majengo yote ya Ghorofa eneo
la Posta yanafungwa Taa na Runinga za Matangazo ili kupendezesha Mji na
kuongeza mwanga nyakati za usiku.
Amesema katika nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani majengo
marefu yamekuwa sehemu ya matangazo hususani nyakati za usiku na kufanya
miji kupendeza hivyo hata Dar es salaam tunaweza kufanya hivyo ili
kufikia azma ya Rais Magufuli kutaka Dar es salaam kuwa mji wa Biashara.
Aidha amesema mradi huo utakuwa wa awamu ili kuhakikisha mitaa
na maeneo ya wazi yanaboreshwa ilikuwafanya wananchi kuwa na maeneo
mengi ya kupumzika na kubadilishana mawazo ikiwa ni maono yake ya Dar es
salaam Mpya.
Awali eneo hilo lililofahamika kama Kaburi Moja lilikuwa
likitumika kama Choo, Maegesho holela na wakati mwingine likitumiwa kwa
uhalifu na uchafu wa mazingira.
Amewataka wananchi kutunza vizuri eneo hilo ili liweze
kuwanufaisha wengi huku akipiga marufuku wamachinga kutofanya biashara
kwenye eneo hilo.
Aidha Makonda amesema anataka kuona vituo vyote vya Daladala
mkoa wa Dar es salaam vinaboreshwe kuwa vya kisasa na kuwa sehemu ya
matangazo ili kupendezesha mji na kuchangia ongezeko la mapato.



0 Comments