BARCA YAKATAA KUMSAJILI MAHREZ
Barcelona wameikataa fursa ya kumsajli Riyad Mahrez kutoka Leicester City, kwa mujibu wa TransferMarketWeb .
MAN CITY YAMTOLEA OFA ALEXIS
Manchester City wanajipanga kutoa kitita cha £60 millioni kwa ajili ya nyota wa Arsenal Alexis Sanchez kwa mujibu wa The Telegraph .
PEREZ ANATAKA KUONDOKA ARSENAL
Lucas Perez yu mbioni kukamilisha uhamisho wake kutoka Arsenal siku
chache zijazo kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 11 kurejea Deportivo
La Coruna, kwa mujibu wa Daily Mail.
CHELSEA YAMTAKA COSTA KUREJEA MAZOEZINI
Diego Costa anayetaka kuondoka Chelsea ameambiwa arejee kwenye
mazoezi ya klabu hiyo ikiwa anataka kupata nafasi kwenye kikosi cha
Antonio Conte, kwa mujibu wa habari kutoka The Sun .
BARCA YAMTENGEA HAZARD €120M
Barcelona wanataka kumsajili Eden Hazard kutoka Chelsea kwa adai ya
uhamisho ya euro milioni 120 majira haya ya joto, kwa mujibu wa Diario Gol .
Real Madrid pia wanataka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa
Ubelgiji lakini Barca bado wanalo tumaini la kuishawishi Chelsea
kumuuza.
BARCA KUONGEZA OFA YA COUTINHO
Barcelona hawatakata tamaa kumsajili Philippe Coutinho na wapo tayari
kutoa dau nono la paundi milioni 137 kuishawishi Liverpool kufanya
biashara, limeripoti Sun .
Miamba hao wa Catalan wamechachamaa wakitaka kumsajili mchezaji huyo
tangu kuondoka kwa Neymar, lakini Liverpool bado wakingali kusita
kumuuza.
ASENSIO KUIZUNGUMZIA ARSENAL KWENYE MKUTANO WA DHARURA
Mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio atafanya mazungumzo ya
dharura na klabu yake kuhusu uhamisho kwenda Arsenal, kwa mujibu wa The Mirror .
Gunners wanapambana kufikia dau la paundi milioni 72 kumsajili
Muhispania huyo, lakini bado pia yumo kwenye rada za Manchester United,
City na Liverpool na Barcelona pia lakini atabaki Bernabeu ikiwa atapewa
mkataba mpya.
WILSHERE ATAKIWA NEWCASTLE
Newcastle United wamejipanga kumsajli mchezaji wa Arsenal ambaye amekosa ushawishi Emirates Jack Wilshere kwa mujibu wa Sun .
MBAPPE KUIGHARIMU PSG ZAIDI YA NEYMAR
Paris Saint-Germain wipata saini ya Kylian Mbappe kutoka Monaco kwa bei kubwa kuliko ile ya Neymar, limeripoti The Times.
Miamba hao wa Ligue 1 walitumia euro milioni 220 kumsajli Neymar kutoka Barcelona.
0 Comments