Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akionyesha moja ya jezi
zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo l;a chalinze Ridhiwani Kikwete.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo hilo
zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za
wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
vifaa hivyo Ridhiwani, amesema kuwa atawapatia washindi wa pili wa
michuano hiyo pikipiki ya miguu miwili na jezi kwa timu zote tatu za
juu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Bagamoyo Majid Mwanga,ambaye pia ndio muaandaji wa mashindano hayo
ametoa zawadi ya pikipiki ya Toyo ya miguu mitatu kwa mshindi wa
kwanza ili itumike kwa shughuli za kuwaingizia kipato kwa vijana.
Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete leo amegawa vifaa vya
michezo kwa timu za jimbo la Chalinze zinazoshiriki mashindano ya kombe
la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya Bagamoyo. Hapa picha
mbalimbali zikionyesha Mbunge huyo akigawa vifaa vya michezo kwa
viongozi mbalimbali wa vilabu vya mpira katika jimbo hilo.






0 Comments