Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo Ndg.John L.Kayombo kwa kushirikiana na Team kutoka TANROAD na mkandarasi wa ujenzi wa Ubungo Interchange wamefanya ziara katika eneo la Mradi wa
ujenzi wa Interchange kwa lengo la kukagua eneo la Mradi ambalo lina vibanda na
wafanyabiashara ambao watalazimika kuondolewa ilo kupisha ukamilishaji wa mradi
huo .
Mradi wa Interchange kwa Manispaa ya Ubungo
ulizinduliwa Rasmi na Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli tarehe 20/3/2017
ikiwa ni moja ya juhudi ya serikali katika kuboresha miundo mbinu ya barabara
ili kurahisisha usafirishaji na kuchochea mapinduzi ya viwanda utakaopelekea ukuaji wa uchumi ,pia kulifanya jiji la Dar
es salaam kuwa la kisasa zaidi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano
-UMC




0 Comments