Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (katikati)
akipata maelekezo ya jinsi kifaa cha kieletroniki cha kubaini magonjwa ya
magari kinavyofanya kazi kutoka kwa Fundi Yakubu Kibingo wa karakana ya MT.
Depot. Kushoto kwa Waziri ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu. Mhandisi Masauni alifanya ziara ya siku moja katika
karakana hiyo mapema leo, ili kujionea jinsi matengenezo ya magari ya serikali
yanavyofanyika.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (wa
pili kushoto) akimsikiliza meneja wa Karakana ya MT. Depot, Mhandisi Julius
Humbe alipo kuwa akifafanua jambo, kuhusu taratibu za matengenezo ya magari ya
serikali. Mhandisi Masauni alifanya ziara ya siku moja katika karakana hiyo mapema
leo, ili kujionea jinsi matengenezo ya magari ya serikali yanavyofanyika.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa kwaza kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.
Mhandisi Hamad Masauni (katikati). Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa
Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Sylvester Simfukwe. Mhandisi Masauni
alifanya ziara ya siku moja katika karakana hiyo mapema leo, ili kujionea jinsi
matengenezo ya magari ya serikali yanavyofanyika.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni
(katikati) akifafanua jambo kwa watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
alipotembelea karakana ya MT. Depot mapema leo, ili kujionea matengenezo ya
magari ya Serikali yanavyofanyika katika karakana hiyo. Kushoto kwa Waziri ni
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu na kulia kwake ni Mkurugenzi wa
zalishaji na matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe.
Mafundi wa Karakana ya MT. Depot wakifanya matengenezo
kwenye gari, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni,
aliyetembelea karakana hiyo mapema leo ili kujionea jinsi magari ya serikali
yanavyotengenezwa.
Picha na TEMESA





0 Comments