Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga
akizungumza na wadau wa Asasi za Kirai nchini na Waandishi wa Habari Mjini
Dodoma katika uzinduzi wa uhakiki wa Asasi za Kiraia Agosti 21,2017.
Msajili wa
Asasi zisizokuwa za kirai Bw. Marcel Katemba akisisitiza jambo kuhusu mwitikio
chanya uliooneshwa na mashirika hayo katika uandaaji wa uhakiki wa Mashirika
Yasiyokuwa ya Kiserikali katika kikao na waandishi wa habari mkoani Dodoma Agosti
21,2017.
Mwenyekiti wa
Baraza la Asasi za Kiraia Tanzania Bw. Nicholous Zakaria akipongeza azma ya
Seriklai kuendesha uhakiki wa mashirika yasiyokuwa ya kireikali katika kikao cha
uzinduzi wa zoezi hilo mkoani Dodoma Agosti 21,2017.
Mwenyekiti wa
Maandalizi ya Uhakikiki wa Asasi zisizokuwa za Kiserikali Bw. Onesmo Olenguruma
akielezea kuridhishwa na ushirikishwaji wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiseriklai
katika kuendesha uhakiki wa mashirika hayo hapa nchini Agosti 21,2017.
Katibu Mkuu Baraza
la Asasi za Kiraia Tanzania Bw. Ismail Suleiman akisisitiza kuendeleza
mashirikiano katika kufanikisha uhakiki wa mashirika yasiyoya kiserikali ambao
katika kiako cha uzinduzi kilichofanyika mkoani Dodoma Agosti 21,2017.
Baadhi ya wadau
kutoka Asasi za Kirai nchini, watendaji wa Wizara na waandishi wa Habari
wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa uhakiki wa
mashirika yasiyo ya kiserikali uliozinduliwa mkoa Dodoma Agosti 21,2017.
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga
akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa asasai zisizo za kiserikali muda mfupi
baada ya uzinduzi wa kazi ya uhakiki wa mashirika hayo hapa nchini Agosti
21,2017.
Picha na Erasto Ching’oro
WAMJW
......................................
Na
Raymond Mushumbusi WAMJW
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Sihaba
Nkinga amewashauri wamiliki wa Asasi za kiraia (NGOs) kutumia fursa ya muda
uliotolewa na Wizara kuhakiki asasi zao na wale ambao hawajasajili asasi zao
kuzisajili.
Ametoa
ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizindua mpango wa kuhakiki Asasi zisizo
za kiraia unaoanza Agosti 21, 2017 na kumalizika Septemba 4, 2017.
Ameongeza
kuwa suala la kuhakiki Asasi za kirai ni la muhimu na litapelekea kupata kubaini
asasi hizo nchini na mchango wao kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
“Niyaombe
yale mashirika ambayo yanafanya kazi za NGO’S na hayakusajiliwa kwa mujibu wa
Sheria ya NGOs yatumie fursa hii kujisalimisha na kujisajili’’ alisema Bibi
Sihaba.
Aidha
kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Asasi za Kiraia Tanzania Bw. Nicholous
Zakaria ameishukuru Serikali kwa kuchukua hatua nzuri ya kuhakiki Asasi hizo
ili kupata taarifa zilizo sahihi kuhusu asasi hizo kwa maendeleo ya asasi,
jamii na taifa kwa ujumla.
“Nichukue
fursa hii kuipongeza Serikali kwa ushirikiano mnaotupatia kupitia Waziri, Katibu Mkuu na Msajili wa Asasi za kiraia
katika kufanikisha shughuli zetu za kila siku” alisema Bw. Nicholous Zakaria.
Katika
kuhakikisha zoezi la uhakiki linafanikiwa na kuwafikia wadau wengi zaidi Wizara
imegawa uhakiki katika Kanda tano ambazo ni Kanda ya Mashariki itakayohudumia
mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Morogoro na Pwani, Kanda ya Kati itakayohudumia
mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida, na Dodoma, kanda ya Ziwa itakayohudumia mikoa
ya Geita, Shinyanga, Mara, Kagera na Mwanza, Kanda ya kasikazini itakayohudumia
mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, Kanda ya Nyanda za Juu itahudumia
mikoa ya Katavi, Rukwa, Ruvuma, Njombe,
iringa na Mbeya.
Aidha, mmiliki wa asasi anaweza kupata huduma ya usajili
katika kituo kitakachokuwa karibu ili kufanikisha zoeezi la uhakiki ambalo
litatoa sura halisi ya idadi, shughuli na mchango wa kisekta katika maendeleo
ya Taifa.










0 Comments