Waziri Wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akizungumza na wafanyabiashara
wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
(JNIA), wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu
MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim
Msangi (Kulia), wakati alipokagua sehemu ya kuingilia abiria katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
Wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere (JNIA) wakimsikiliza Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa (Hayupo pichani) wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri Wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafanyabiashara
wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
(JNIA), wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
...............................
Waziri Wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa Mwezi mmoja kwa
wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere (JNIA) kulipa kodi ya Majengo kama mikataba yao inavyolekeza.
Waziri Mbarawa ametoa
agizo hilo leo wakati alipokutana na wafanyabiashara hao ili kujadili
changamoto mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzitatua ili kuendelea kutoa huduma
bora katika uwanja huo.
“Kulipa kodi za
majengo hapa ni suala la lazima, hivyo ifikapo Septemba mwishoni nataka kuona
wafanyabiaashara wote mmeshalipa kodi ya pango, makusanyo haya ni muhimu kwetu
ili tuendelee na hatua nyingine za uboreshaji wa viwanja vya ndege na huduma
nyinginezo.” Amesisitiza Profesa Mbarawa.
Aidha, Profesa Mbarawa
ameutaka uongozi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Kuhakikisha
mikataba yote ya upangishaji wa majengo inapitiwa upya na kufanyiwa marekebisho
ili thamani ya fedha iendane na wakati huu.
Profesa Mbarawa
amewahimiza wafanyabiashara hao kubadilika na kuendana na mabadiliko ya Sayansi
na Teknolojia ili kuweza akuendana na ushindani wa kibiashara uliopo ndani na
nje ya nchi.
Ameongeza kuwa
Serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri kwa wafanyabiashara nchini ili
waweze kufanya biashara zao ili kujiingizia kipato binafsi na kukuza pato la Taifa.
Katika hatua nyingine
Profesa Mbarawa amekagua sehemu ya kuingilia abiria katika uwanja huo ambapo
amesema Serikali itaweka mpango maalum wa muda mfupi kwa wasafiri wanaoenda nje
kutotumia muda mrefu katika ujazaji wa fomu wakiwa uwanjani hapo.
“Kwa kushirikiana na
taasisi zote zinazotoa huduma katika uwanja huu tutaweka mpango maalum utakaowezesha wasafiri
kuhudumiwa kwa haraka na kwa muda mfupi, Msafiri yoyote anataka huduma za
haraka ili waweze kuwahi na sisi tutahakikisho tunakidhi mahitaji ya wateja,”
amesisitiza Profesa Mbarawa.
Kwa upande Kaimu
MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim
Msangi amesema Mamlaka imeshapitia mikataba yote ya wafanyabiashara kiwanjani hapo
na hatua inayofata ni kufatilia madeni yote ili kuboresha huduma katika kiwanja
hicho.
Bw. Msangi ameongeza
kuwa kwa yale madeni ambayo hayataweza kulipwa kwa wakati taratibu za kisheria
zitafuatwa.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.




0 Comments