Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasanii wa Nyimbo za Injili (hawapo
pichani) wakati wa mkutano na wasanii hao kujadili changamoto zinazowakabili na
namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Chama cha Hakimiliki Tanzania
(COSOTA) Bibi. Doreen Sinare akifafanua jambo wakati wa mkutano na wasanii wa
nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua
changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania
(CHAMWITA) Bw. Addo Novemba akiwasilisha changamoto zinazokabili muziki wa
injili hapa nchini wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili
changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es
Salaam.
Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bi. Christina Shusho
akichangia hoja wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili
changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es
Salaam.
Waimbaji wa nyimbo za Injili wakitumbuiza wakati
wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na
namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati)
katika picha ya pamoja na viongozi kutoka serikalini pamoja na viongozi wa
chama cha Muziki wa Injili Tanzania baada ya mkutano na wasanii hao kujadili
changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es
Salaam.
Picha
na:
Genofeva Matemu - WHUSM
.................................
Na: Genofeva Matemu –
WHUSM
Waziri Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe amekutana na wasanii wa
nyimbo za Injili leo Jijini Dar es Salaam kusikiliza changamoto zinazoikabili
tasnia ya muziki wa nyimbo za injili na kuweka mikakati ya kuzitatua changamoto
hizo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza wakati wa
mkutano na wanamuziki wa nyimbo za Injili Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali
ina wajibu wa kufuatilia changamoto za tasnia ya muziki ukiwemo muziki wa
injili na kuzitatua ili kuweza kukuza kazi za wasanii kwa maslahi ya mtu mmoja
mmoja na taifa.
“Muziki ni tasnia
ambayo imewabeba vijana wengi hapa nchini, serikali ina wajibu wa kutetea, kulinda
na kuhakikisha maslahi ya kazi za sanaa ikiwemo muziki wa injili inaheshimiwa
na kulindwa” Amesema Mhe. Mwakyembe
Kwa upande wake
Katibu Mtendaji Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare
amewataka Wasanii wa Muziki wa Injili kutoshawishiwa kutoa malipo yoyote katika
vyombo vya habari ili nyimbo zao ziweze kuchezwa kwenye vyombo hivyo bali
vyombo vya habari ndio vinapaswa viwalipa wasanii wakati wanapotumia nyimbo
zoa.
Aidha Bibi. Doreen
amewaomba waimbaji hao wa nyimbo za injili kutembelea ofisi za Bodi ya Filamu,
Cosota na Basata ili waweze kupata ushauri wa namna ya kuandika mikataba bora
na inayofaa wakati wa kutengeneza na kuandaa albamu za nyimbo za injili.
Naye Rais wa Chama
cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMWITA) Bw. Addo Novemba amewataka Viongozi wa
nyimbo za Injili Tanzania kuhakikisha kuwa wanafanya kazi bega kwa bega na
serikali na kwa bidii katika kukuza, kuendeleza, na kulinda maslahi ya
wanamuziki wa Injili.
Aidha Bw. Novemba ameiomba
serikali kuhusisha wanamuziki wa nyimbo za injili katika matukio mbalimbali ya
serikali na ya nchi kwani wasanii wa nyimbo za injili wamekua wakiimba nyimbo
zinazojenga taifa na kuendeleza amani, upendo na ushirikiano wa nchi yetu.






0 Comments