Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akizungumza na Vyombo vya Ulinzi
na Usalama ambapo vyombo hivyo viko tayari kushiriki ujenzi wa Ofisi za
walimu wakuu pamoja na vyoo katika shule za msingi na sekondari zenye
mahitaji ya huduma hizo.
......................
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mheshimiwa Paul Makonda leo ameelezea Dhamira yake ya kuhakikisha ujenzi
wa Ofisi za kisasa 402 za walimu pamoja na Vyoo kwa shule za Msingi na
Sekondari zilizobainika kuwa upungufu wa huduma hizo.
Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na sehemu ya Chumba cha Mwalimu
Mkuu,Chumba cha Muhasibu, Chumba cha Katibu Muktasi pamoja na ofisi za
Msaidizi wa Mwalimmu mkuu na walimu wote huku zikiwa na Vyoo vya kisasa
pamoja na Bafu.
“Siwezi kuwa na amani kama walimu wangu hawana ofisi wala
vyoo katika shule 402, ni haibu na fedhea kwa walimu kugombania choo na
mwanafunzi au kutumia vyoo vya majirani au Bar, hii sio heshima ya
mwalimuwa Mkoa wangu,ndio maana nimeamua kuanza kufanyia kazi changamoto
hizi,” Alisema Makonda.
Kutokana na gharama za ujenzi kuwa kubwa Mheshimiwa Makonda
ameviomba vyombo vya Ulinzi na usalama vya Mkoa wa Dar es Salaam
kumpatia mafundi wa ujenzi kama sehemu ya kuunga mkono jitiada
alizoanzisha za ujenzi wa Ofisi hizo ambapo vyombo hivyo vimeridhia
kumuunga mkono.
“Kipekee napenda kuvipongeza vyombo vyote ya Ulinzi
vilivyoamua kuniunga mkono vikiongozwa na Mkuu wa JKT kwa utayari wa
kunipa vijana watakaofanya ujenzi huo, na niwaeleze kuwa ujenzi utaanza
baada ya wiki mbili zijazo” Aliongeza Makonda.
Ujenzi wa Ofisi hizo unategemea zaidi jitiada za wadau wa
maendeleo ikiwemo wamiliki wa kampuni pamoja na Wananchi wenye dhamira
ya kuona Walimu wanafanya kazi katika mazingira Mazuri.
Tayari jitiada za Mheshimiwa Makonda zimeanza kuzaa matunda
baada ya kufanikiwa kupata Mabati 11,000 na mifuko ya Saruji 1,000
ambapo Mahitaji ni Mabati 50,000, Mbao zaidi ya Million mbili pamoja na
vifaa vingine vya ujenzi.
Makonda amesema ataanza kutembelea viwanda vinavyojihusisha
na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi ikiwemoMabati, Saruji, Nondo na
vinginevyo kuona namna wanavyoweza kuunga mkono ujenzi huo ili
kuhakikisha walimu wanafanya katika mazingira rafiki


0 Comments