Dar
es Salaam, TANZANIA. Serikali ya Marekani kupitia Taasisi ya kijeshi ya Walter
Reed (WRAIR) imesaini upya makubaliano ya ushirikiano na Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) siku ya Jumanne, Agosti 29, 2017 katika sherehe ya kusaini
tamko la pamoja la ushirikiano katika jitihada za kupambana na VVU/UKIMWI.
WRAIR ni kitengo cha kikosi cha jeshi la Marekani kinachojihusisha na tafiti za
kitabibu na kimefanya kazi moja kwa moja na JWTZ tangu mwaka 2004 kutekeleza
programu za VVU/UKIMWI Tanzania.
Utiaji
saini huo uliofanywa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dr. Inmi
Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja Generali (Dk.)
Denis Raphael Janga, unawakilisha dhamira ya pamoja katika upatikanaji endelevu
wa huduma za afya na mpango mkakati wa kukabiliana na tishio la VVU/UKIMWI.
Makubalino
ya awali, yaliyosainiwa mwaka Aprili 2011 yanabainisha ushirikiano wa pande
hizo mbili katika kupunguza maambukizi mapya na kuboresha matibabu na huduma za
kuzuia maambukizi.
Kupitia
ushirikiano huu endelevu wa pande hizi mbili Mfuko wa Dharura wa Rais wa
Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) unatoa nafasi kwa majeshi ikiwemo JWTZ
kuelewa vizuri tishio la afya, tabia na mazingira hatarishi yanayohusiana na
kuenea kwa maambukizi ya VVU.
“Mafanikio
ya ushirikiano wa WRAIR/JWTZ hayapingiki na faida zake ziko wazi.”alisema Kaimu
Balozi Patterson. “Kwa pamoja tumehakikisha upatikanaji endelevu wa huduma za
tiba kupitia ujenzi wa vituo vipya, ukarabati wa vituo vya zamani, vya matunzo
na tiba na kutoa vifaa vya maabara.”
Ushirikiano
huu wa pande mbili kati ya WRAIR na JWTZ umeundwa kuimarisha na kusaidia
utafiti na utekelezaji wa jitihada za matunzo na matibabu ya VVU nchini
Tanzania.




0 Comments