Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Irenius
Ruyobya akizungumza leo na Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo
wa mwaka 2017 wakati wa mafunzo ya wakufunzi hao yanayoendelea kufanyika mkoani
Morogoro. Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 unatarajia kufanyika nchi
nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.
Mtalaamu wa Kilimo na Mifugo kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na
Uvuvi, Zanzibar Mzee M. Mzee akiwafundisha Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa
Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya wakufunzi hao yanafanyika mkoani
Morogoro ambapo utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi
Oktoba, 2017.
Mmoja wa Wakufunzi akiuliza swali wakati wa mafunzo ya Wakufunzi wa Wadadisi wa
Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 yanayofanyika mkoani Morogoro. Utafiti huo wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017
unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.
Baadhi ya Wakufunzi wakijifunza mbinu mbalimbali zitazotumika kuwafundishia
Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya wakufunzi hao
yanafanyika mkoani Morogoro ambapo utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima
kuanzia mwezi Oktoba, 2017.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius
Ruyobya akitoa maelekezo kwa waratibu wa mafunzo ya Wakufunzi wa Wadadisi wa
Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya Wakufunzi hao yanafanyika
mkoani Morogoro na utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi
Oktoba, 2017.
(PICHA ZOTE NA VERONICA
KAZIMOTO)
................
Na:
Veronica Kazimoto Mororgoro
Jumla ya wakufunzi 52 wakiwemo Mameneja Takwimu
wa mikoa yote nchini wamepewa mafunzo juu ya mbinu mbalimbali zinazotumika
kufundishia wadadisi kwa ajili ya kupata takwimu bora za kilimo na mifugo.
Mafunzo hayo ya wiki moja yanayoendelea
kufanyika mkoani morogoro, yanalenga kuwajengea uwezo wakufunzi hao ili waweze
kuwafundisha wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa Mwaka 2017 kwa ajili ya
kupata takwimu rasmi zitakazotumika katika kupanga mipango ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius
Ruyobya amewataka wakufunzi wao kuzingatia kwa makini mafunzo hayo ili waweze
kuwafundisha kwa ufanisi wadadisi wakaokusanya taarifa za utafiti huo wa kilimo
na mifugo.
"Ili kuiwezesha nchi yetu kupata
takwimu bora za kilimo na mifugo inatakiwa ninyi wakufunzi kuzingatia kwa
makini mafunzo haya ili muweze kuwafundisha kwa ufanisi mkubwa wadadisi ambao
watazunguka nchi nzima kukusanya takwimu za kilimo na mifugo", amesema
Ruyobya.
Utafiti wa Kilimo na Mifugo hufanyika kila
mwaka ambapo utafiti wa mwaka huu utafanyika kuanzia mwezi Oktoba, 2017 chini
ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi na Wizara ya Viwanda na Biashara.





0 Comments