Baadhi ya mazao ya Misitu zikiwemo mbao ambazo zitakuwa zikukusanywa kwa njia ya
kielektroni kupitia mfumo wa ukusanyaji
maduhuli uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na Mipango unaoitwa Government electronic
Payment Gateaway-GEPG ikiwa ni kutii agizo la Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ya kuzitaka Taasisi za serikali kujiunga na
mfumo huo.
.....................................
.....................................
Picha na Lusungu Helela
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanza utekelezaji
wa ukusanyaji wa maduhuli kwa njia ya kielektroniki kufuatia marekebisho ya
sheria ya fedha ya mwaka 2017 na maelekezo ya serikali ya awamu ya tano ambao
umezitaka Taasisi za serikali kujiunga na mfumo wa ukusanyaji maduhuli
uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na Mipango unaoitwa Government electronic
Payment Gateaway-GEPG.
Akitoa ufafanuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Mhasibu Mkuu
wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Peter Mwakosya amesema mashamba yote na
ofisi za mameneja (DFM's) wa Taasisi hiyo zimeunganishwa katika mfumo
huo.
Aidha amesema kutokana na mazingira ya
vizuia(checkpoints) kutokidhi mahitaji ya mfumo huo na hasa kushindwa
kuhifadhi vitendea kazi kama kompyuta na printa kwa sasa wakala inaendelea
kuunganisha kwenye mfumo vizuia vyote kwa kutumia vifaa maalum (point of
sales-POS).
Amebainisha kwamba vifaa hivyo vitatumika kukusanya maduhuli
na kuhakiki uhalali wa nyaraka zinazokaguliwa katika vituo vyote vya ukaguzi wa
mazao ya misitu na nyuki kwa kipindi hiki ambacho vinaendelea kuunganishwa vizuia kwenye mfumo
wa moja kwa
moja.
Mwakosya amesisitiza maduhuli
yote yatakayokusanywa kwenye vizuia yanawasilishwa Ofisi za mameneja wa Misitu
wa wilaya mapema ili yaingizwe kwenye mfumo.
Pia amewakumbusha
wateja wote wa Mazao ya Misitu na nyuki kuzingatia kwamba wanatakiwa kupata hati
za madai (Bill) katika mfumo kabla ya kwenda kufanya
Malipo.
Aidha, amewakumbusha wateja wa bidhaa za Misitu na nyuki
kwamba stakabadhi zilizokuwa zikitumika kabla ya mfumo huo (ERV) hazitaendelea
kutumika katika vituo vilivyounganishwa na mfumo.

0 Comments