
Kenyatta akipiga kura
LEO
ni siku ya uchaguzi nchini Kenya na Wakenya wengi wamejitokeza kupiga
kura. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 11:00 asubuhi. Mpaka
sasa, wagombea wanaochuana vikali, Odinga na Kenyatta, wamepiga kura
katika maeneo tofauti.

Odinga akipiga kura.
Rais
Uhuru Kenyatta amepiga kura kwenye shule ya msingi ya Mutomo na
amesikika akiwaomba Wakenya wote wafanye uchaguzi huo kwa amani.

Kenyatta akipiga kura.
Upande mwingine, Odinga amepiga kura katika shule ya Kibra, Nairobi. Ikumbukwe kuwa Odinga anagombea kwa mara ya nne sasa.

Habari zaidi kinachoendelea katia uchaguzi huo zitaendelea kukufikia hapahapa.
0 Comments